Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai 2013. Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Marais mbalimbali na Wajumbe zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unalenga kuwanufaisha Watanzania kiuchumi, kiteknolojia na kijamii. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kushoto) na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.