Monday, May 20, 2013

Mhe. Membe azungumza na Mabalozi kuhusu Mkutano ujao wa Smart Partnership

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai 2013. Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Marais mbalimbali na Wajumbe zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unalenga  kuwanufaisha Watanzania kiuchumi, kiteknolojia na kijamii. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kushoto) na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini, Mhe. Juma  Khalfan Mpango.

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Manufaa kwa Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013)

Mabalozi wengine wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (kushoto, mstari wa kwanza) na Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage pamoja na baadhi ya Mabalozi wakimsiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

Meneja wa Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Manufaa kwa Wote (Smart Partnership Global Dialogue 2013), Bibi Rosemary Jairo akiwaeleza Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa (hawapo pichani) hatua zilizofikiwa katika kuandaa mkutano huo.

Picha zaidi za baadhi ya Mabalozi waliohudhuria Mkutano huo.

Baadhi ya Mabalozi wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Bibi Jairo (hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya mkutano huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na Bw. Japhet Mwaisupule, Afisa Mambo ya Nje Mkuu wakati wa mkutano kati ya Mhe. Membe na Mabalozi.

Mkuu wa Sekrtarieti ya Maandalizi ya Mkutano huo hapa nchini, Bibi Victoria Mwakasege (kushoto) akiwa  na Bibi Jairo wakati wa mkutano wa Mhe. Membe na Mabalozi.

Picha zaidi za mkutano kati ya Waziri Membe, Mabalozi na Wakuu wa Masharika ya Kimataita waliopo hapa nchini


Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo yake na Mabalozi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Sekretarieti ya Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote, Bibi Mwakasege (kulia) na Meneja wa Maandalizi ya Mkutano huo Bibi Jairo (kushoto).

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.