Friday, April 30, 2021
BALOZI MULAMULA ATEMBELEA WATUMISHI WALIOPO KATIKA JENGO LA PSSSF
Wednesday, April 28, 2021
TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA MAZURI WAWEKEZAJI WA MAREKANI
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Serikali
ya Tanzania imewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani mazingira
mazuri na kuwasihi kuendelea kuwekeza hapa nchini.
Ahadi
hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa
Marekani nchini Mhe. Donald Wright katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam.
Balozi
Mulamula amesema makampuni mbalimbali kutoka Marekani yameonesha nia ya
kuwekeza katika sekta za nishati, miundombinu, afya na kilimo hususani katika
zao la korosho.
“Katika
kikao changu na Balozi tumejadili na kusisitiza umuhimu wa Kampuni za Marekani
kuwekeza nchini Tanzania.........na Balozi amenihakikishia baadhi ya kampuni
hizo zipo tayari kuwekeza hapa nchini,” amesema Balozi Mulamula
Aidha,
Mhe. Waziri Mulamula amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania
kujipanga kutumia fursa ya kuuza Marekani bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa
nchini.
Kwa
Upande wake Balozi wa Marekani, Mhe. Wright amesema uhusiano wa Marekani na
Tanzania ni wa miaka mingi na kuahidi kuuendeleza na kuimarisha uhusiano huo.
“Suala
la wawekezaji kuja kuwekeza hapa Tanzania nimemhakikishia Mhe. Waziri kuwa
suala la wafanyabishara na wawekezaji wa Kimarekani kuja kuwekeza hapa Tanzania
ni jambo ambalo nimelipa kipaumbele na ninalifanyia kazi kwa karibu ili
wawekezaji wa Kimarekani waendelee kuja kuwekeza kwa wingi Tanzania,” amesema
Balozi Wright
Katika
tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Mulamula amekutana kwa maongezi na Balozi wa Comoro hapa nchini, Mhe.
Dr. Ahmada El Badasui pamoja na Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN),
Bw. Zlatan Milišić ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano.
“Tumekubaliana
kukutana na tume za ushirikiano ili tuweze kujadili na kuona ni jinsi gani
tunaweza kuboresha masuala ya biashara na ushirikiano katika maeneo
mbalimbali,” amesema Waziri Mulamula.
Nae
Balozi wa Comoro hapa nchini amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania na
kuhakikisha uhusiano huo unaendelea kwa maslahi ya pande zote mbili.
“Leo
nimepokelewa na Waziri Mulamula na tumejadiliana masuala ya ushirikiano baina
ya Comoro na Tanzania na pia tumeongelea masuala mbalimbali yanayohusu mabalozi
hapa Tanzania pamoja na maeneo ambayo tutaanza kuyafanyia kazi kati ya Comoro
na Tanzania,” amesema Mhe. El Badasui.
Kwa
upande wake Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Milišić
amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili
kuhakikisha inafanikisha malengo ya maendeleo endelevu iliyojiwekea katika
kuwaletea maendeleo watanzania.
“UN
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inafanikisha agenda zake
za maendeleo endelevu,” amesema Bw. Milišić.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akiongea na Balozi wa Comoro hapa nchini, Mhe. Dr. Ahmada El
Badasui wakati wa maongezi yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar es Salaam
Balozi
wa Comoro hapa nchini, Mhe. Dr. Ahmada El Badasui akimuelezea jambo Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakati
wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN),
Bw. Zlatan Milišić katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Mratibu
Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Zlatan Milišić akimueleza jambo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) wakati wa maongezi yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam
Tuesday, April 27, 2021
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA BURUNDI, UINGEREZA NA UMOJA WA ULAYA
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na mabalozi watatu wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na kupokea nakala ya hati za utambulisho za balozi mteule wa Italia hapa nchini.
Mabalozi hao wamekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Burundi Mhe. Gervais Abayeho, Balozi wa Uingereza Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo Fanti.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu Biashara na Uwekezaji na Utamaduni.
“Leo nimekutana na mabalozi watatu kutoka Burundi, Uingereza na Umoja wa Ulaya na nimejadiliana nao masuala mbalimbali ya ushirikiano katika masuala ya uchumi, biashara na uwekezaji na mahusiano baina yetu na nchi zao,” amesema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula ameongeza kuwa “mabalozi wote watatu wameahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia kwa manufaa ya nchi zetu………lakini pia tumejadili mipango ya kimkakati kutoka kwa Umoja wa Ulaya na Uingereza ambapo wangependa kuona inaendelezwa katika awamu hii,” amesema Balozi Mulamula.
Nae Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Abayeho amesema uhusiano wa Burundi na Tanzania ni wa miaka mingi na wamefurahia kuuona uhusiano huo ukiendelea kuboreka zaidi na tunaamini uhusiano huo utaendelea kudumu kwa miaka mingi.
“Uhusiano wa Burundi na Tanzania ni uhusiano wa muda mrefu na tunafurahia kuona unazidi kuimarika. Mbali na masuala ya uhusiano umependekeza utekelezwaji wa miradi mikubwa kama vile ujenzi wa bandari, barabara na reli uharakishwe kwa manufaa ya nchi zote mbili,” Amesema Balozi Abayeho
Kwa upande
wake Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar amesema katika kikao
chake na Mhe. Waziri wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Uingereza
na Tanzania na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha na kuendeleza
uhusiano huo.
Katika tukio jingine, Mhe. Waziri Mulamula amepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Italia hapa nchini Mhe. Marco Lombardi.
“Tanzania na Italia tuna uhusiano mzuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo utalii, uwekezaji na elimu na tumejadiliana mambo aliyoagizwa na serikali yake katika kudumisha uhusiano wa Italia na Tanzania.
Kwa Upande wake Balozi Mteule, Mhe. Lombardi amesema Italia na Tanzania zina masuala mengi ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi,kijamii na utamaduni na kwamba yuko nchini kuhakikisha hayo yote yanatekelezeka kwa maslahi ya nchi zote mbili.
“Tunaamini kupitia maongezi yetu ya leo tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu wa kiuchumi na kisiasa kwa maslahi ya Italia na Tanzania, lakini pia nimemhakikishia Mhe. Waziri kuwa Italia itaendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania katika kuhakikisha mahusiano yake ya kidiplomasia yanakua na kuimarika,” amesema Mhe. Lombardi
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Manfredo Fanti wakati
wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akimsikiliza Balozi wa Burundi hapa nchini Mhe. Gervais Abayeho wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akimsikiliza Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Italia
hapa nchini Mhe. Marco Lombardi jijini Dar es Salaam
|
Monday, April 26, 2021
BALOZI LIBERATA MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA,UFARANSA,ISRAEL,UBELGIJI NA UJERUMANI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Frederick Clavier mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharika Jijini Dodoma. Mazungumzo hayo yalilenga kudumisha mahusiano baina ya chi hizo mbili katika Nyanja za diplomasia ya mahusiano na uchumi,biashara na uwekezaji
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa Nchini Balozi Oded Joseph mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma. Katika mazungumzo hayo Balozi Mulamula amemsihi Balozi Oded kuhakikisha Israel inakuwa na Ubalozi wake rasmi hapa Nchini na kumshukuru kwa hatua ya Israel kuwachukuwa vijana wa Kitanzania kwenda Nchini humo kwa mafunzo ya vitendo na nadharia kuhusu kilimo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji hapa Nchini Balozi Peter Van Acker mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma. Mazungumzo hayo yalilenga pamoja na mambo menfine ukamilishwaji wa majadiliano ya ushirikiano katika sekta ya usafiri wa anga na kuimarisha ushirikiano katika sekta za kilimo na usambazaji wa maji safi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Regina Hess mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma. Pamoja na masumla menfine Viongozi hao walijadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya afya,elimu,biashara,uwekezaji pamoja na maliasili na utalii
Sunday, April 25, 2021
NAIBU WAZIRI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA KAMATI YA SERIKALI YA URUSI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), akiagana na Balozi Oleg Ozerov, Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali ya Urusi inayosimamia Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), akiwa katika mazungumzo na Balozi Oleg Ozerov, Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali ya Urusi inayosimamia Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. |
Friday, April 23, 2021
BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA AFYA LA AHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA AFYA
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Jamii Mhe. Christophe Bazivamo (kulia) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya, Sekretarieti ya Jumuiya Dkt. Michael Katende wakiratibu Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya. |
Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea jijini Arusha Tanzania |
Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea jijini Arusha Tanzania |
Kaimu Mkurugezi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kushoto) akifuatilia Mkutano wa kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya uliokuwa ukiendelea jijini Arusha, Tanzania. |
Washiriki wa Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. |
Thursday, April 22, 2021
ANGLOGOLD ASHANTI, TANZANIA ZAKUBALIANA KUENDELEZA USHIRIKIANO
Na Mwandishi wetu, Dar
Kampuni
ya Madini ya Anglogold Ashanti ya Afrika Kusini imeahidi kuendeleza ushirikiano
na Serikali ya Tanzania katika sekta ya madini na kuhakikisha kuwa sekta hiyo
inakuwa mstari wa mbele kuchangia uchumi.
Ahadi
hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika, Bw. Sicelo
Ntuli wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) leo Jijini
Dar es Salaam.
Akiongea
mara baada ya mazungumzo hayo Balozi Mulamula amesema kuwa, Anglogold Ashanti
ni wadau wakubwa katika sekta ya madini na wameonesha utayari wao wa kushirikiana
kwa karibu na Serikali katika kukuza na kuendeleza sekta ya madini.
“Leo
hii nimekutana na uongozi wa Kampuni ya Madini ya Angogold Ashanti na
tumejadili pamoja na mambo mengine, utayari wa Kampuni hiyo kushirikiana na
Serikali katika kukuza sekta ya madini hapa nchini,” Amesema Balozi Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa kitendo cha kukutana na wadau wa madini kama Anglogold
Ashanti na kujadiliana nao masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kukuza sekta ya
madini ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Kwa
Upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti Bw. Ntuli amesema kuwa
uongozi wa Anglogold umefarijika kukutana na Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na
kuweza kujadiliana nae mambo mbalimbali ikiwemo suala la kukuza ushirikiano
baina ya Kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania.
“Sisi
kama Anglogold tumefarijika kuona Serikali ya Tanzania ipo tayari kuendeleza
ushirikiano na Sisi…….tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa maslahi mapana
ya pande zote mbili,” Amesema Bw. Ntuli
Aprili 16, 2021 Kampuni ya Anglogold Ashanti iliingia ubia na Kampuni ya BG Umoja ya nchini Tanzania kwa ajili ya kuchimba madini katika miradi ya Nyankanga na Geita Hill. Anglogold ni Kampuni mama ya Geita Gold Mine (GGML) imeipatia BG Umoja mkataba wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 186 kwa miaka miwili.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika,
Bw. Sicelo Ntuli wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika, Bw. Sicelo Ntuli akimueleza jambo Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akiongoza kikao chake na Kampuni ya Madini ya Anglogold Ashanti
ya Afrika Kusini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam
Wednesday, April 21, 2021
MKUTANO WA KAWAIDA WA 20 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA AFYA UNAENDELEA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA, TANZANIA.
Kaimu Mkurugezi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akichangia jambo kwenye Mkutano wa kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaoendelea kufanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania. |
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt.Leonard Subi akifuatilia mkutano wa kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania. |
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt.Leonard Subi akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaoendelea kufanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania
|
Ujumbe kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano |
Mkutano wa kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania. |
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA AFRIKA KUSINI
Na Mwandishi
wetu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe.
Grace Naledi Pandor kujadili mambo ya kuendeleza mashirikiano baina ya Jamhuri
ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Mulamula amefanya mazungumzo hayo Pretoria nchini
Afrika Kusini ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula alieleza kuwa
mahusiano kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni ya kihistoria na yameendelea
kuimarika tangu enzi a kupigania uhuru kwa nchi za kusini mwa Afrika.
Kwa upande wake Waziri Pandor ameishukuru kwa ujio
wa Balozi Mulamula na kwa kufika nchini Afrika Kusini na pia alieleza kuwa
Jamhuri ya Afrika Kusini inathamini mashirikiano ya kihistoria kati ya nchi
zetu mbili na hivyo kinachohitajika ni kuendeleza na kuimarisha mashirikiano ya
kiuchumi na kisiasa tuliyonayo sasa hivi. Jamhuri ya Afrika Kusini inayo azma
ya kushiriki kikamilifu kujenga makumbusho ya urithi (heritage museum) ya
harakati za kupigania uhuru kusini mwa Afrika zenye chimbuko lake nchini
Tanzania na vilevile kuonyesha juhudi za Tanzania katika harakati za kupigania
uhuru na kwa nchi za kusini mwa Afrika.
Mawaziri hao wamejadili pia mchakato wa tathimini
ya utekelezaji wa Bi-National Commission (BNC) ambapo kwa mwaka huu Afrika
Kusini ndiyo itakuwa mwenyeji wa tathimini hiyo ambayo hujumuisha ngazi ya
watedaji wakuu wa sekta mbalimbali wan chi hizi mbili, Mawaziri na huitimishwa
na Waheshimiwa Marais wa nchi zote mbili.
Aidha, Balozi Mulamula kabla ya kukutana na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, alikutana na watumishi wa ubalozi wa Tanzania
Pretoria katika mkutano ulifanyika Ubalozini, Mhe. Waziri alipokea taarifa ya
eneo la uwakilishi la Ubalozi ambalo linajumuisha Afrika Kusini, Botswana,
Falme ya Lesotho na SADC. Taarifa hiyo ilieleza juhudi za Ubalozi katika kukuza
mahusiano na nchi za eneo la uwakilishi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa
diplomasia ya uchumi, diplomasia ya siasa, wanadiaspora wa eneo la uwakilishi.
Balozi Mulamula ameutaka Ubalozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini kuendela kufanya kazi kwa malengo, watumishi kujiwekea malengo ili
kufanikisha malengo ya Ubalozi na hatimaye Ubalozi kuchangia malengo ya Wizara
kwa ujumla.
“Nawasihi kuendeleza mahusiano na nchi za
uwakilishi na Balozi nyingine zilizopo katika nchi za uwakilishi na suala hili
la kujenga mahusiano na watumishi wote na siyo Balozi pekee yake,” amesema
Balozi Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Pretoria nchini Afrika Kusini. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Grace Naledi Pandor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Grace Naledi
Pandor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo