Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Dovitoglu ambapo alimuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kwa awamu nyingine kuiwakilisha Jamhuri ya Uturuki nchini. |
Friday, December 29, 2017
Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uturuki nchini
Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini
Mhe. Waziri Mahiga akielekezana jambo na Mhe. Song Geum-Young. |
Mhe.Waziri Mahiga akiagana na Mhe Song Geum-Young. |
Thursday, December 21, 2017
Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China
Dkt. Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu vingi sana. |
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China akiuliza sawali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga. |
Picha ya Pamoja. |
Ziara katika kampuni ya magari ya Foton Motors Group
Baadhi ya aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya karakana ya Foton Motors Group kuangalia shughuli za uzalishaji wa magari zinavyofanyika. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea zawadi ya mfano wa moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. |
Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant
Tuesday, December 19, 2017
China yaunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Na Mwandishi Maalum, Beijing
China imeahidi kushirikiana na Tanzania
kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya AwamuyaTano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo
2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Hayo yalibainishwa leo jijini Beijing na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian
Keming na baadaye kukaririwa tena na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC), Bw. Ning
Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Katika mazungumzo hayo,
Balozi Mahiga aliainisha na kufafanua namna Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt.
John
Pombe Maguful iilivyokusudia kuwashirikisha wadau mbalimbali kwenye utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ambayo inalenga kuchochea
agenda ya uchumi wa viwanda.
Miradi hiyo ni pamoja na kuendeleza nishati ya umeme ambapo Serikali imedhamiria kuzalisha umeme wa
megawatts 5000 ifikapo mwaka 2020 ili kuharakisha utekelezaji wa agenda
ya uchumi wa viwanda ambayo haitaweza kufanikiwa kama hakutakuwa na umeme wa kutosha na wauhakika.
Kutokana na uhalisia huo, Serikali imepanga kujenga kituo cha
kuzalisha umeme wa megawatts 2100 kwenye mto Rufiji
na kujenga njia za kusambaza umeme huo kutoka Rufiji, Chalinze hadi Dodoma
na nyingine kutokaChalinze, Kilimanjaro hadi Arusha.
Miradi mingine ni ujenzi wa mtandao wa usafiri wa reli na uboreshaji wa reli ya
TAZARA,
ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na viwanja vya ndege ikiwa ni pamoja na kujenga jengo la abiria katika Kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Waziri
Mahiga alisisitiza umuhimu wa miundombinu hiyo kuunganishwa ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa katika uchumi.
Aliongeza kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa wastani wa asilimia 7
kwa mwaka na uchumi wa nchi za jirani ambazo zinategemea bandari za Tanzania pia unakua,
hivyo kuendeleza na kuunganisha miundombinu ya usafiri ni muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi hizo na uchumi wa
Tanzania.
Aidha, Waziri Mahiga alieleza namna Serikali inavyoendelea na zoezi
la kuhamisha makao makuu ya Serikali kwenda Dodoma na kukaribisha makampuni ya China
kushiriki kwenye uwekezaji wa miundombinu mbalimbali kwenye mji huo mpya wa makao makuu.
Baadhi ya miundombinu muhimu inayohitajika Mjini Dodoma ni upatikanaji wa maji safi ya na ya uhakika na kuiomba
China ishiriki katika ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro.
Bwawa hilo likijengwa na kukamilika litasaidia sio tu kusambaza maji ya uhakika mkoani
Dodoma bali hata mkoa wa Dar Es Salaam ambao matumizi ya maji yanaongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kila siku.
Waziri
Mahiga aliahidi kuwa Serikali yake itakamilisha taratibu zilizosalia ili mradi wa Mchuchuma na Liganga uweze kuanza kwa kuwa mradi huo ni muhimu sana katika
sera ya uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Biashara aliahidi kuwa Serikali ya
China itafanyia kazi kwa haraka miradi yote iliyowasilishwa ili Tanzania
iweze kutimiza malengo yake ya kuwaletea maendeleo wanachi.
Aliongeza kuwa Serikali yake itaharakisha kufanya upembuzi yakinifu wa miradi hiyo kwa madhumuni ya kutimiza masharti ya kampuni za uwekezaji na taasisi zinazotoa fedha nchini
China.
Aidha, alipongeza hatua ya Serikali ya Tanzania
ya kuweka mikakati ya kuzalisha umeme wa megawatts 5000 ifikapo mwaka 2020. Hivyo,
aliahidi kuwa atazishawishi kampuni za China zinazozalisha umeme wa jua,
upepo na joto ardhi zijek uwekeza nchini ili lengo hilo litimie kwa haraka.
Wakati huo huo, Waziri Mahiga alikutana na watendaji wa makampuni mbalimbali ya uwekezaji yaliyodhamiria kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali.
Makampuni hayo yanataka kuwekeza kwenye uzalishaji wa Sukari, ujenzi wa kiwanda cha
kusindika mihogo, uagizaji wa mihogo mikavu toka Tanzania kwa wastani wa tani laki 3
hadi 5 kwa mwaka na huduma za kitalii kama ujenzi wa mahoteli yenye hadhi ya nyota tano.
Kampuni hizo zote zimeomba kukutanishwa na wadau husika ili wkamilishe taratibu zinazotakiwa waanze uwekezaji haraka iwezekanavyo.
Waziri Mahiga aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa uamuzi wao wa kuwekeza
Tanzania hawataujutia kwa kuwa Tanzania ni nchi tulivu na yenye amani,
ina rasilimali nyingi na soko kubwa kutokana na kuwa mwanachama wa SADC na EAC.
Matukio yanayojiri katika ziara ya kikazi ya Balozi Mahiga nchini China
Wajumbe wa pande mbili za China na Tanzania wakiwa katika mazungumzo. |
Balozi Mahiga akitoa zawadi ya picha kwa Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming. |
Mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango ya China
Ujumbe wa Tanzania na China wakijadiliana namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiano katika masuala ya uchumi, uwekezaji n biashara. |
Bw. Jing Jizhe akionesha utayari wa nchi yake wa kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi. |
Balozi Mahiga na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China. |
Balozi Mahiga akiwa na katika mazungumzo na mmoja wa wawekezaji aliyedhmiria kuwekeza Tanzania. |
Mwekezaji mwingine akisalimiana na Balozi Mahiga kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao. |
Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt, Lu Youqing |
Mhe. Balozi, Dkt. Ramadhani Dau awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme wa Cambodia
Mhe. Balozi Dkt. Dau (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mtukufu Mfalme mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Wanaoshuhudia kulia ni maafisa wa Serikali ya Cambodia na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania. Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 1995. Pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji. Vilevile Mtukufu Mfalme aliahidi kumpa ushirikiano Mhe. Balozi Dkt. Dau katika utekelezaji wa majukumu yake. |
Mhe. Balozi Dkt. Dau akimtambulisha Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Bw. Khatib Makenga aliyeambatana naye katika hafla ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho |
Mhe. Balozi Dkt. Dau akipokelewa mara baada ya kuwasili jijini Phnom Penh, Cambodia. |
Thursday, December 14, 2017
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ampokea Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi alipowasili uwanja wa ndege wa mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi katika Ikulu ndogo ya Mjini Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao |
Wednesday, December 13, 2017
TANZIA
TANZIA
Marehemu Mama Badriya Kiondo |
Familia za Bw. Kiondo wa Kwaminchi Tanga na Bw. Ramadhan Haji wa Betras, Zanzibar wanasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa, Bi. Badriya Ramadhan Kiondo aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini India kilichotokea tarehe 11 Desemba, 2017 katika Hospitali ya Apollo mjini New Delhi, India.
Mwili wa Marehemu Mama Kiondo unatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2017 saa 8.45 mchana kwa Ndege ya Shirika la Emirates. Aidha, mazishi yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 saa 10.00 jioni.
Msiba wa Marehemu Mama Kiondo upo nyumbani kwa mumewe Bw. Frank Mwamkai Kiondo maeneo ya Ada Estate, Na. 73, Kinondoni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Ufaransa.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia hizi popote pale walipo.
Tuesday, December 12, 2017
Waziri Mahiga awaasa Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Wazalendo na kusimamia maslahi ya Jumuiya.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba 2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah Makame. |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi. |
Mwenyekiti wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wake. |
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho. |
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao hicho. Kutoka kulia Bw. Eliabi Chodota, Bw. Bernard Haule na Bw.Joachim Otaru. |
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi akitoa ufafanuzi kuhusiana na taratibu na miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waheshima Wabunge Wateule. |
Mhe. Waziri na Naibu Waziri wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Picha ya pamoja uongozi wa Wizara na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Subscribe to:
Posts (Atom)