Tuesday, July 28, 2020

HAFLA YA MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA- HAYATI BENJAMIN MKAPA



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali wilbert Ibuge(wa kwanza kushoto), akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya Uhuru kwa ajili ya kuongonza hafla ya Kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania Mhe. Hayati Benjamin William Mkapa, aliyefariki dunia tarehe 24 Julai 2020, Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi(aliyesimama mwisho kulia), akisoma wasifu wa Mhe, Hayati Mkapa.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Jenerali Alain                   Guillaume Bunyoni, akitoa salam za rambirambi kutoka Nchi ya        Burundi, Jenerali Bunyoni pia ameambatana na Spika wa Bunge la    Nchi hiyo pamoja na viongozi wengine kutoka nchini humo.

Kiongozi(Dean) wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, Balozi wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mabalozi wenzake. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe          Magufuli akihutubia viongozi na wananchi waliohudhuria hafla ya    Kitaifa ya kumuaga Rais wa awamu ya tatu, Mhe. Hayati Mkapa.   
  akiongea katika hotuba yake alisisitiza Watanzania kuenzi mambo      mengi mazuri aliyoyaacha Hayati Mkapa, Mhe. Magufuli alisema      "Ninamshukuru Mungu kwa zawadi ya Maisha ya Mkapa".

 Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania Nje ya nchi  pamoja  na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania (waliosimama mistari mitatu ya mwisho) wakiwa katika hafla hiyo

   Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini
   ( mistari miwili ya mwisho) wakifuatilia shughuli hiyo


       Mawaziri waliohudhuria wakifuatilia shughuli hiyo


   Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat                Mfumukeko( wa pili kulia), akiongozwa na Afisa Itifaki Bw. Ishengoma kuingia uwanjani kushiriki shughuli hiyo

    Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakitoa heshima     za mwisho kwa mwili wa Hayati Mkapa

         Mabalozi wakiendelea kutoa heshima za mwisho


     Mabalozi wakiendelea kutoa heshima za mwisho

  Mhe. Kabudi akimuaga Mhe. Magufuli alipokuwa akitoka uwanjani

   Mhe. Kabudi akiagana na Waziri Mkuu wa Burundi, Mhe. Bunyoni


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika                  Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro(Katikati),                              akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.                  Hamad Masauni(Kulia), baada ya hafla hiyo kumalizika

    








Monday, July 27, 2020

WAZIRI KABUDI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA BURUNDI NA UJUMBE WAKE





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi, Jenerali Alain Guillaume Bunyoni alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria mazishi ya Kitaifa ya Hayati Benjamin William Mkapa, yatakayofanyika tarehe 28 Julai 2020, Viwanja vya Uhuru, Jijini Dar es Salaam



Mhe. Kabudi na Mhe. Jenerali Bunyoni wakiwa katika mazungumzo katika chumba maalum cha viongozi (VIP), Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, tarehe 27 Julai 2020

Sunday, July 26, 2020

HABARI KATIKA PICHA MABALOZI WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KWA RAIS MSTAAFU MZEE MKAPA


Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wameendelea kujitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na kumuelezea kuwa ni kiongozi mahiri na msuluhishi nguli wa amani barani Afrika na duniani.


Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Dissing-Spandet akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam

Balozi wa Hispania nchini Mhe. Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Bw. Michael Sulusi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa  

Mwakilishi wa Ubalozi wa Uganda nchini Bibi. Musekura Eseza akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa  

Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa  

Mwakilishi wa Ubalozi wa Sudan nchini Bw. Jaafar Nasir Abdalla akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Balozi wa Somalia nchini Mhe. Mohamed Hassan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Balozi wa Congo DRC nchini Mhe. Jean-Pierre Mutamba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Mwakilishi wa Ubalozi wa Uturuki nchini Bw. Onur Yay akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa

Baadhi ya mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na mama Anna Mkapa mara baada ya kutoa salamu za pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam  

Saturday, July 25, 2020

MABALOZI 'WAMLILIA' RAIS MSTAAFU MZEE MKAPA


Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wamejitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam 'wakimlila' na kumuelezea kwa mema mengi aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

Mabalozi hao walianza kuwasili nyumbani kwa Mzee Mkapa kwa nyakati tofauti ambapo mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo baadhi yao wakaelezea walivyoguswa na msiba.

Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa amemuelezea Mzee Mkapa kuwa alikuwa mtu makini na aliyependa    masuala ya kidiplomasia.   

"Nimekuja hapa kwa niaba ya Serikali ya Misri kuja kutoa pole kwa kuondokewa na Mzee Mkapa kiongozi mchapakazi kwa taifa la Tanzania na alikuwa kiongozi aliyeinua uchumi wa taifa ambapo chini ya uongozi wake Tanzania iliingia katika ubinafsishaji na utandawazi", Amesema Balozi Abulwafa.

Ameoneza kuwa Mzee Mkapa atakumbukwa na wanadiplomasia wengi duniani kwani alikuwa kiongozi aliyependa amani ambapo enzi za uhai wake alisuluhisha mauaji ya kimbari katika nchi za Rwanda na Burundi pamoja na kurejesa amani katika nci za Sudan, Kongo DRC, Zimbabwe na Kenya.

"Tutamkumbuka kwa upendo na uchapakazi wake uliokuwa umetukuka na kuonesha matunda ya amani na mandeleo kwa Tanzania na Afrika Mashariki", Amesema Balozi Abulwafa.

Kwa upande wake mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald amemuelezea Rais Mstaafu Mzee Mkapa kuwa alikuwa rafiki mkubwa wa Ireland, na ambaye aliyeendeleza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ireland ambao hadi sasa upo imara.

"Kwetu sisi kama Serikali ya Ireland tumeguswa sana na msiba huu, kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi na mpenda amani….daima tutamkumbuka kwa mema yaka na uchapaji kazi wake ulioiletea Tanzania maendeleo. Tulimfaamu vizuri alikuwa kionozi mpenda maendeleo na amani……kwetu sisi ni pigo kubwa sana kwa kifo chake" Amesema Fitzgerald

Baadhi ya mabalozi waliofika na kusaini kitabu cha maombolezo ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi, Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa, Balozi wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan, Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe.  Ally Abdallah Almahruqi.


Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam  

Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam  

Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa Marehemu jijini Dar es Salaam  


Balozi wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa


Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe.  Ally Abdallah Almahruqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam  

Mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyomfahamu Rais Mstaafu Mzee Mkapa wakati alipokuwa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam

PROF. KABUDI AMLILIA MZEE MKAPA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa. Mhe. Benjamin William Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa ya Julai 24,2020 Jijini Dar Es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lupaso,Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Jumatano ya Julai 29,2020

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa. Mhe. Benjamin William Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa ya Julai 24,2020 Jijini Dar Es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lupaso,Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Jumatano ya Julai 29,2020

Thursday, July 23, 2020

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI AKARIBISHA KIWANDA CHA NYAYA CHA CAIRO KUWEKEZA NCHINI

Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Meja Generali (Mst.) Anselm Shigongo Bahati akifanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Giza Power kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya pande mbili. Kampuni hiyo inamiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbalimbali.  Kadhalika, Mhe. Balozi Bahati alitembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho  na kujadili na uongozi wa kiwanda hicho kuhusu kuja kuwekeza Tanzania. Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.
Mhe. Balozi Bahati akipata maelezo kutoka kwa mtaalam alipokitembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbalimbali. Kwenye ziara hiyo Mhe. Balozi Bahati alijionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho. Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.

Tuesday, July 21, 2020

Naibu Katibu Mkuu Dkt Haji akaribishwa rasmi Wizarani



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Dkt Mwinyi Talib Haji katika ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma,  mara baada ya kuapishwa tarehe 20 Julai 2020.

Menejimenti ya Wizara wakiwa wamejipanga kumkaribisha ofisini Naibu Katibu Mkuu Dkt Haji ofisini Mtumba.

Naibu Katibu Mkuu akisalimiana na sehemu ya Menejimenti

Naibu Katibu Mkuu akisalimiana na sehemu ya Wakurugenzi, kulia ni Katibu Mkuu Balozi Ibuge akiwa emeongozana nae. 



                      Naibu Katibu Mkuu akisalimiana na sehemu ya Wakurugenzi

Katibu Mkuu Balozi Ibuge akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu alipomkaribisha ofisini kwake Mtumba, Dodoma.





Thursday, July 16, 2020

DKT. NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Wilaya hiyo Mhe. Christina Mndeme ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika baada kuhitimisha ziara iliyofanywa na Dkt. Ndumbaro ya kutembelea mipaka inayoinganisha Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji iliyopo katika Mkoa wa Ruvuma. 

Dkt. Ndumbaro kwa nyakati tofauti katika mwaka huu amefanya ziara maalumu katika mpaka wa Magazini uliopo Wilayani Namtumbo-Ruvuma, Wenje uliopo Wilayani Tunduru-Ruvuma, Chiwindi uliopo Wilayani Nyasa-Ruvuma  na baadaye mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini. Mipaka yote inaiunganisha Tanzania na Nchi jirani ya Msumbiji. 

Lengo la kufanya ziara ilikuwa ni kubaini na kutatua changamoto zinazokabili maeneo ya mipakani sambamba na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Katika ziara hizo Dkt. Ndumbaro alikutana na kuafanya mazungumzo na baadhi ya wananchi na watumishi katika mipaka husika. Sambamba na changamoto kadhaa alizozibaini aliridhishwa na utendaji wa Watumishi waliopo mpakani na kuwahimiza kundelea kufanyakazi kwa bidii,ubunifu na kwa kuzingatia maadali.

Aidha, Dkt. Ndumbaro katika kikao chake na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Ruma amebainisha kuwa changamoto nyingi zilizoelezwa mipakani zikiwemo ukosefu wa umeme, barabara za kiwango cha lami, mawasiliano na Vituo vya kutoa huduma Pamoja Mpakani (OSBP), Serikali chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tayari zimeanza kufanyiwa kazi.

Dkt. Ndumbaro kwa upande wake amehimiza umuhimu wa Mamlaka za Mkoa hasa zilizopo maeneo ya Mipakani kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, kudumisha na kulinda uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe. Christina Mndeme kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, amempongeza Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro kwa ziara hiyo na jitihada anazifanya katika kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi inaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Mhe. Christina Mndeme wakisalimia walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipo wasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mideme
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akifafanua jambo alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma.

Kikao kikiendelea