Monday, May 30, 2016

Press Release


 
PRESS RELEASE
RE: POSITION OF LEGAL ADVISER (DIRECTOR) AT THE ORGANISATION FOR THE PROHIBITION OF CHEMICAL WEAPONS (OPCW)

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation through its Embassy in the Netherlands has received a notification from the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW) stating that the position of Legal Adviser (Director) will be vacant in August 2016.

The Legal Adviser will be responsible for the provision of legal advise to the Director General of OPCW, the Technical Secretariat, the policy making organs and States Parties to the Convention.

The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply. Closing date for application is on Tuesday 30th May, 2016.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dar es Salaam.
30th May, 2016

Friday, May 27, 2016

Stars watua Nairobi kuwakabili Harambee

Balozi Haule akiongea na Wachezaji wa timu ya Taifa. Kulia ni Kocha Mkuu Boniface Mkwasa na wa pili kushoto ni Mshauri wa timu Abdallah 'King' Kibadeni. 
Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza Balozi Haule.
Balozi Haule katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa Stars

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Mhe. Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa waadilifu, kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa na  kuifanya Tanzania kuendelea kupaa katika medani za kimataifa.
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi ya mkutano kwa Mhe. Waziri, Viongozi wa TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo  kumkaribisha Mhe. Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
   
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika utendaji wa kazi.
Mjumbe kutoka TUGHE-Taifa, Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kuwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa taarifa ya wafanayakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo 

Afisa Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri Mahiga na Wafanyakazi bora wa Idara zote za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa Kimataifa kujadili Utawala wa Sheria kufanyika nchini
Mkutano wa Kimataifa kujadili masuala ya Utawala wa Sheria kama chachu ya Maendeleo Endelevu unatarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 1 na 2 Juni, 2016.
Mkutano huo ambao utafanyika katika ngazi ya Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika utafunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe (Mb.) na kuhudhuriwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika, Maafisa Waandamizi wa Serikali na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa.
Mkutano huo unaolenga kuweka sera, mikakati thabiti, pamoja na kubadilishana uzoefu, weledi na ujuzi miongoni mwa washiriki ili kuwawezesha kutekeleza malengo mapya ya dunia chini ya dira mpya ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Dunia ijulikanayo kama “Agenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030” yenye jumla ya Malengo 17. Malengo hayo yanarithi Malengo ya Milenia yaliyomaliza muda wake mwaka 2015.
Ikumbukwe kuwa, mwezi Septemba 2015 Jumuiya ya Kimataifa ilifikia makubaliano ya kihistoria kwa kupitisha Agenda mpya ya Maendeleo Endelevu wakati wa Mkutano Maalum wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Mjini New York, Marekani. Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa walikubaliana kuwa na Dira Mpya ya Maendeleo ya Dunia ikilenga katika kutokomeza umaskini; kulinda mazingira; kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kushirikisha makundi yote kwenye jamii katika masuala ya maendeleo.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sheria (International Development Law Organisation-IDLO) yenye Makao yake makuu mjini Roma, Italia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki takriban 70 kutoka ndani na nje ya Tanzania na umejikita zaidi kwenye lengo Namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 27 Mei 2016.

Waziri Mahiga apokea msaada wa magari ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini

Waziri wa Mambo ya nje Ushirikano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (aliye shikilia funguo za gari), akipokea Ufunguo wa Magari ya Wagonjwa kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini, Mhe. Song Geum Young  yaliyotolewa Serikali ya nchi yake. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo Kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo ambo utatumika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza.  Tanzania na Korea Kusini zina mahusiano mazuri, ambapo Korea Kusini inaendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya,miundombinu, elimu na uchumi.
Waziri Mahiga akijaribisha moja ya magari aliyokabidhiwa na Serikali ya Korea Kusini kupitia Balozi Young kushoto.
Picha ya Magari yaliyotolewa kwa msaada wa Serikali ya Korea Kusini
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kusini Mhe. Song Geum Young mara baada makabidhiano ya magari kwa Mhe. Dkt. Mahiga (hayupo pichani) 


Picha na Reginald Philip

Thursday, May 26, 2016

EAC tables USD 100 M Budget to EALA

Hon Dr Susan Kolimba, Deputy Minister, Foreign Affairs and East African
Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko.

The deputy Minister of Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the
EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.

Tanzania na China kuendelea kuimarisha ushirikiano

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwaonyesha waandishi wa habari  kitabu kinachoelezea Historia ya Ushirikiano baina ya Tanzania na China kwenye Mkutano na vyombo vya habari  uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ambao  Bi. Kasiga aliwaelezea mafanikio ya ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima nchini China  ambapo  pamoja na kufadhili shughuli mbalimbali za kiuchumi, nchi hiyo pia imekubali kutoa ufadhili wa nafasi kumi za masomo ya kidiplomasia ambapo itatoa nafasi tano za  mafunzo ya muda mrefu na tano za muda mfupi kwa kila mwaka
Mkutano ukiendelea
==================================================================



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ziara ya Kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini China

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima alifanya ziara ya kikazi nchini China kuanzia tarehe 15 – 19 Mei 2016 kufuatia mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na China katika nyanja za siasa, uchumi na utamaduni.

Akiwa nchini China, Dkt. Mlima pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Makampuni makubwa ya China ambayo baadhi yao yameshawekeza nchini na mengine yameonesha dhamira ya kuwekeza.

Wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Zhang Ming, masuala mbalimbali yalijitokeza ikiwa ni pamoja na China kusisitiza dhamira yake ya dhati ya kukuza ushirikiano na Tanzania katika nyanja ya uchumi kupitia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, nishati na miundombinu. China imeweka kipaumbele cha juu katika miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda pamoja na maboresho ya Reli ya TAZARA na ipo tayari kuanza upembuzi yakinifu wa Reli ya Kati. 

Kwa upande wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Kampuni ya China ya Merchant Holding International (CMHI) ambayo imeingia ubia na Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Oman kujenga bandari hiyo, wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha mazungumzo ya ubia wao ili waanze awamu ya kwanza ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ndani ya mwaka huu wa 2016.
Kwa suala la ujenzi wa eneo la viwanda, Serikali ya China imebainisha kuwa ikwishatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu wezeshi (barabara, nishati ya umeme, maji, TEHAMA).

Kuhusu Reli ya TAZARA, China imeahidi kuwa itaendelea kuipa kipaumbele cha juu reli hiyo kwa sababu inabeba historia ya mahusiano yake na Afrika. China imeridhishwa na mazungumzo ya wataalamu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuahidi kufanyia kazi yaliyokubalika ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kupitia Itifaki ya 16 kwa ajili ya maboresho makubwa ya miundombinu ya TAZARA pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye mikutano itakayofuata kuangalia namna bora ya kuendesha reli hiyo kwa ushirikiano na Tanzania na Zambia. 

Mkutano na Mamlaka ya Tumbaku

Katibu Mkuu alikutana na Kamishna wa State Tobacco Monopology, Bw. Lin Chengxing ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia utekelezaji wa Mkataba wa Kuruhusu Tumbaku ya Tanzania kuingia soko la China uliosainiwa mwaka 2013 wakati Rais wa nchi hiyo, Mhe. Xi Jinping alipofanya ziara nchini. Bw. Lin alijulisha kwamba makampuni mawili ya China-Hunan Industries na Shandong Industries yamepewa jukumu la kuinunua tumbaku ya Tanzania kwa ajili ya kufanya majaribio. 

Hadi hivi sasa wameshanunua tani 1500 ambazo zinahifadhiwa kwa kati ya miezi 24 hadi 30 (fermentation) kabla ya kutumika kuzalisha sigara. Matarajio yao ni kwamba sigara zitakazozalishwa na tumbaku ya Tanzania itaingia soko la China mwaka ujao. Endapo soko la China litapendelea sigara hizo, mahitaji ya tumbaku ya Tanzania katika soko la China yataongezeka kwa kiasi kikubwa. 

Mkutano na Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje

Dkt. Mlima alikutana na Rais wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China, Prof. Qin Yaqing ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya chuo hicho na Chuo cha Diplomasia cha hapa nchini. Katika majadiliano hayo,  walikubaliana kushirikiana katika tafiti na utoaji wa mihadhara.  Aidha, Chuo hicho kimeahidi kutoa nafasi za masomo tano za muda mfupi na tano za muda mrefu kila mwaka kwa Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje. Chuo hicho kilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China na baadaye kilianzisha programu mbalimbali na kuchukua wanafunzi kutoka nje ya nchi. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 26 Mei 2016.