Ujumbe ulioshiriki kikao hicho ukisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu. |
Mkutano ukiendelea. |
Ujumbe ulioshiriki kikao hicho ukisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu. |
Mkutano ukiendelea. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Nchi za Kiafrika
zimeiomba China kuhakikisha kuwa ufadhili ama mikopo inayotoa kwa Nchi za
Kiafrika inalenga katika miradi ya kikanda itakayoziunganisha na kuzinufaisha
nchi hizo kiuchumi huku Tanzania ikiitaka China kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo
inayowekeza nchini iwe ya manufaa kwa pande zote mbili.
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
ameyasema hayo Beijing Nchini China katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la
ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) alipopata fursa ya kuzungumza
katika mkutano huo na kuongeza kuwa endapo China itazisaidia kwa ufadhili ama
kwa mikopo nafuu kuwekeza katika miradi hasa ya miundombinu itakayoziunganisha
Nchi za kiafrika kwa kiasi kikubwa itazisaidia Nchi hizo kufanya biashara
zenyewe kwa zenyewe itaziwezesha kupiga
hatua za kimaendeleo na kiuchumi na hivyo kujitegemea.
Ameongeza kuwa
Mkutano huo wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika
(FOCAC) umekuwa ni wa manufaa kwa kuwa Nchi zenyewe za kiafrika zimepata fursa
ya kutaja baadhi ya miradi ya kipaumbele kutokana na uhitaji wa Nchi husika huku akiitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na
uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji kwa kuwa Nchi nyingi za Kiafrika bado zina
vyanzo vingi vya maji vinavyoweza kuzalisha umeme ambao utakuwa ni wa bei nafuu
na kusaidia katika ujenzi wa viwanda.
Aidha, katika
mkutano huo wa siku mbili uliozikutanisha Nchi zipatazo 53 za Kiafrika na China
zimeitaka China pia kuhakikisha inasaidia ama kufadhili katika kuinua uwezo wa
kitaaluma utakaowawezesha vijana kwa Kiafrika kujiajiri na kupata wataalam
wabobezi katika masuala mbalimbali kutokana na uwekezaji hasa wa viwanda na
miundombinu utakaofanywa kwa pamoja na China na Nchi za Kiafrika.
Akizungumza mara
baada ya kumalizika kwa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amesema katika mkutano huo wa
waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Tanzania
imesisitiza kuwa katika miradi ya uwekezaji ya misaada ama ile ya mikopo nafuu
inayoelekezwa Tanzania iwe ni ile yenye manufaa kwa pande zote mbili yaani win-win situation kama anavyosisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
Akisoma hotuba
kwa niaba ya Rais wa China Mhe. Xi Jimping, Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Mhe. Wang Yi amesema kuwa China haitatoa misaada yenye masharti magumu kwa Nchi
za Afrika, badala yake itaendeleza ushirikiano wake na Afrika katika kutekeleza
miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa pande zote mbili.
Katika hotuba
hiyo, Serikali ya China imeahidi kuongeza umoja na ushirikiano kati yake na
Afrika katika masuala ya kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na kudumisha
amani na usalama ili kuleta maendeleo
endelevu kwa watu na kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi.
Mkutano huo wa
waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika limeazimia kwa pamoja
kutekeleza miradi ya kipaumbele kulingana na uhitaji wa kila nchi kwa kufuata
hatua nane zilizotangazwa katika mkutano wa wakuu wa nchi wa FOCAC uliofanyika
mwezi September 2018 jijini Beijing.
Hatua hizo ni
pamoja na program ya kuendeleza viwanda kupitia ujenzi wa maeneo maalum ya
viwanda, ujenzi wa miundombinu ikiwemo nishati, reli, barabara na
bandari, sambamba na ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vitakavyosaidia kuzalisha
nguvu kazi ya viwandani.
Imetolewa
na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
BEIJING -
CHINA.
25 Juni 2019
| ||
Meza kuu watatu kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ni mgeni wa heshima na Mkuu wa Nchi pekee kutoka Bara la Afrika akiwa katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika. Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje China na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi. Mkutano huo umefanyika Beijing,China na Kuhudhuriwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Nchi za Afrika 53. Juni 25, 2019.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) (watano kutoka kushoto) akiwa katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaohudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje 53 kutoka Nchi za Afrika. Mkutano huo unafanyika Beijing – China. Juni 25, 2019. |
Sehemu ya Mawaziri wa mambo ya Nje kutoka Nchi 53 za Afrika wanaohudhuria mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).Mkutano huo unafanyika Beijing – China. Juni 25, 2019. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake akiwa kwenye mkutano pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi na ujumbe wake. Mkutano huo umefanyika Beijing,China. June 24, 2019. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi na ujumbe wake mara baada ya kumaliza mkutano baina yao. Mkutano huo umefanyika Beijing,China. June 24, 2019. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni sitini bila ya masharti yeyote pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Bw. Zhou Liujun,akisaini kwa niaba ya serikali ya China. Zoezi hilo limefanyika Beijing,China. June 24, 2019. |
| ||
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 53 za Afrika na taasisi za fedha za China. |
Sehemu ya mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na wajumbe wao waliohudhuria katika wamkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 53 za Afrika na taasisi za fedha za China. Beijing,China. June 24, 2019. |
Dodoma, 24 Juni 2019
Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ulipokea kifaa
muhimu cha kufundishia madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa sekta ya afya,
pamoja na vitabu vya kitabibu kutoka katika Jumuiya ya Watanzania waishio
Uingereza wanaofanya kazi katika sekta ya afya (Tanzania United Kingdom Health
Diaspora Association - TUHEDA). Makabidhiano hayo yalifanyika jijini London tarehe 22 Juni 2019.
Kifaa hicho ni sanamu ya binadamu ambayo
inaendeshwa na programu maalumu za kompyuta zinazowezesha wataalamu mbalimbali
wa afya kupata uhalisia wa hali ya magonjwa kama ambavyo wangeupata kutoka kwa
mgonjwa aliye hai.
Sanamu hiyo iliyopewa jina la ‘Msafiri’ na Ubalozi, ina
uwezo wa kupumua, kutoa sauti ya mapafu kama mtu mwenye pumu, homa ya mapafu,
au mapigo ya moyo yanayoweza kuashiria shinikizo la juu au la chini la damu,
sawa na mgonjwa halisi. Upatikanaji wa sanamu hiyo umefanikishwa na mwanachama
wa TUHEDA, Dkt. Nasibu Mwande, mtaalamu wa masuala ya ajali na magonjwa ya
dharura (Accidents and Emergency), anayefanya kazi ya udaktari hapa Uingereza.
‘Msafiri’ ana thamani ya pauni za Uingereza zisizopungua 30,000 (sawa na
shilingi za Tanzania zipatazo milioni mia moja), ana umbo la kawaida la
binadamu na uzito wa kilo 60. Ubalozi umetaarifiwa kuwa sanamu hiyo ni ya
kwanza nchini Tanzania katika ufundishaji wa kitabibu.
Kupatikana kwa ‘Msafiri’ kutasaidia sana kupunguza
makosa ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na madaktari, wauguzi na wataalamu
wengine kwani ‘Msafiri’ anaweza kutumika kutoa mafunzo ya kitabibu kwa mfano
halisi wa magonjwa mbalimbali bila ya madhara ambayo yangetokea kama wataalamu
wa utabibu wangetegemea kujifunza kupitia mgonjwa aliye hai.
TUHEDA pia
wamekabidhi vitabu muhimu mia tatu vinavyotumika kama rejea kwa madaktari
wakati wa kuamua mgonjwa apewe dawa gani, dawa zipi zinaweza kutumika kwa
pamoja bila madhara, na zitolewe kwa kiwango gani. Vitabu hivyo vina thamani
inayokaribia pauni 9,000 sawa na shilingi za Tanzania zipatazo milioni 30.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
|
|
Watanzania waishio Uingereza waliohudhuria mapokezi ya Msafiri na vitabu vya utabibu vilivyokabidhiwa na TUHEDA. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania Nchini China na kupokelewa na Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Brighton Kairuki. June 23,2019. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni katika ubalozi wa Tanzania Nchini China. June 23,2019.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni katika ubalozi wa Tanzania Nchini China. Mbele yake anayeshuhudia ni Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Brighton Kairuki. June 23,2019. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika kikao cha pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini China. June 23,2019. |
Ubalozi wa Tanzania Seoul, kwa kushirikiana
na wadau wa Utalii kutoka sekta binafsi wameshiriki katika maonyesho makubwa ya
Kimataifa ya “Seoul International Tourism Industry Fair” yaliyofanyika jijini
Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 6 hadi 9 Juni 2019. Maonesho hayo yaliandaliwa
na Korea World Travel Fair (KOTFA) kwa
kushirikiana na Seoul International
Travel Mart (Seoul Metropolitan City) ambapo wadau (kampuni za utalii,
usafirishaji, wamiliki wa hoteli, migahawa, vyombo vya habari) kutoka nchi
mbalimbali za Asia, Ulaya, Amerika, Afrika na Mashariki ya Kati walishiriki.
Kampuni za Utalii kutoka Tanzania
zilizoshiriki maonesho hayo ni Eastenders, Zara Tours, Travel Booking Guide kwa
kupitia Mwakilishi wake aliye Korea, Ms. Han Bitnarae, na SAFANTA Tours &
Travel ya Zanzibar.
Kupitia maonesho hayo, Tanzania iliweza
kutangaza vivutio vya utalii kwa jamii ya Wakorea na mataifa mengine kwa ujumla.
Aidha, kampuni zilizoshiriki ziliweza kupata wenzao wa kushirikiana nao
kibiashara kupitia B2B na kuingia makubaliano ya kibiashara.
|
Balozi wa Tanzania Korea Kusini,
Mhe. Matilda Swilla Masuka akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Tanzania katika maonesho hayo, pamoja na wageni waliotembelea banda la
Tanzania.
|
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa Maonesho hayo ya Utalii, Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Seoul, na Watanzania waishio Korea Kusini (Diaspora) ambao walikuja kuunga mkono juhudi hizo za kuitangaza Tanzania |
Mwakilishi wa kampuni ya Zara
Tours, Bi Leila Ansell akiongea na wateja kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo
na kampuni hiyo ambayo imeingia mkataba pia na kampuni ya kikorea ya Hyecho
Trekking ambayo hupeleka watu kupanda mlima Kilimanjaro. Mazungumzo pia bado
yanaendelea na makampuni mengine.
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akimsikiliza Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini Bi Janine S. Young alipomwita Wizarani kutoa ufafanuzi kuhusu angalizo la kiusalama lilitolewa na ubalozi huo kupitia tovuti ya Ubalozi wa Marekani hapa Nchini. June 20,2019. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI WAMWITA KAIMU BALOZI WA MAREKANI WIZARANI
Tarehe 19 June, 2019, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania ulitoa taarifa katika mitandao ya kijamii “Twitter” kuhusu angalizo la kiusalama “security alert”. Angalizo hilo la kiusalama lilitokana na uvumi unaodaiwa na ubalozi huo kusambaa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulimwita katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Balozi wa Marekani Bi Janine S. Young ili kutoa ufafanuzi wa “twitter” yao.
Ubalozi wa Marekani ulimtuma Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Janine S. Young kuonana na uongozi wa Wizara ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.
Bi Janine S. Young ameutambua ujumbe huo na kukiri kuwa umetumwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Katika ufafanuzi wake amekiri kuwa Ubalozi umefanya makosa ya kutoa tetesi ambazo hazikuwalenga raia wa Marekani pekee bali raia wote wakitambua kuwa Ubalozi hauna mamlaka ya kufanya hivyo jambo lililosababisha taharuki kwa wananchi na wageni wanaotarajia kuitembelea Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeukumbusha Ubalozi wa Marekani umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za kidiplomasia zinazokubalika duniani kote katika utoaji wa taarifa za aina hii.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amewataka wananchi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na wageni mbalimbali waliopo nchini na wanaotarajia kuitembelea Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa ya kuwepo kwa tishio la aina hiyo hapa nchini na kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejizatiti kukabiliana na matishio yeyote.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam.
20 Juni, 2019
|
Bw. Hassan Mnondwa, Mtumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa ufafanuzi kwa Bw. Abdullatif kuhusu majukumu ya Wizara alipofika kwenye Dawati la Wizara wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Mwingine katika picha ni Mtumishi wa Wizara, Bi. Roxana Kagero. Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo ipo kwa mujibu wa Kalenda ya Umoja wa Afrika, Wizara imefungua madawati maalum kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kusikiliza na kujibu hoja zao kuhusu Wizara pamoja na kueleza majukumu yanayotekelezwa na Wizara. |
Mtumishi wa Wizara akimhudumia mgeni, Bi.Eunice Mmari kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi aliyefika kwenye Dawati la Wizara katika Ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 16 hadi 23 Juni 2019. |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Macha na Deogratius wakiwa tayari kuwapokea na kuwahudumia wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma |
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Jenipher akiwa kwenye dawati lililopo Ofisi za Wizara za Mtumba tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2019 |
Mtumishi wa Wizara akiwa tayari kwenye dawati lilopo Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan. Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund). Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan |
Balozi Mubarak Mohamed Al -Sehaijan pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwait nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani) |
Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan naye akimweleza jambo Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) |
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani) |
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto) |