Friday, February 26, 2016
Waziri Mahiga aongoza maadhimisho ya Siku ya Taifa la Kuwait
Waziri akiendelea kuhutubia |
Balozi Al Najem naye akizungumza katika hafla hiyo. |
Sehemu ya Mabalozi na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakisikiliza hotuba zilizotolewa na Mhe.Dkt. Mahiga na Mhe. Al Najem (hawapo pichani). |
Waziri Mahiga (kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi ambaye alihudhuria hafla hiyo. |
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mhe. Mwinyi. |
Waziri Mahiga kwa pamoja na Balozi Al Najem na Mabalozi wengine wakishiriki kukata keki kama ishara ya kuadhimisha wakati wa hafla hiyo. Anayeshhudia pembeni ni Rais Mstaafu, Mhe.Mwinyi. |
Picha ya pamoja
Picha na Reginald Philip
|
Thursday, February 25, 2016
TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA JPC NA ZAMBIA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi akifungua rasmi Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Zambia. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Zambia, Bi. Angela Mulenga ambaye aliambatana na ujumbe wa maafisa walioiwakilisha Serikali ya Zambia katika Mkutano huo akijadili jambo na Bw. Sylvester Mundanda.
|
Sehemu ya maafisa wa Serikali ya Zambia wakifuatilia Mkutano. |
Sehemu ya maafisa wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia Mkutano.
Serikali za Tanzania na Zambia zinakutana katika kikao cha siku mbili kujadili na kukubaliana maeneo ya ushirikiano ambayo watayasimamia kwa pamoja kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kinachojulikana kama Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) kinafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia leo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Zambia ni mzuri na kufanyika kwa kikao hicho ni uthibitisho dhahiri.
Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa kufanyika kwa kikao hicho kunatoa fursa kwa wajumbe kuchambua kwa pamoja hatua zilizofikiwa na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha 8 cha JPC kilichofanyika Lusaka Juni 2006. Maeneo hayo ni pamoja na biashara, viwanda, mawasiliano, uchukuzi, nishati, uhamiaji, kilimo, elimu, michezo, madini, utalii, maliasili na utamaduni.
“Haya ni baadhi ya maeneo ambayo nchi zote mbili zinayapa umuhimu mkubwa ili kuharakisha maendeleo ya pande zote mbili Katika majadiliano yetu tutalenga zaidi maeneo haya ili tubuni utaratibu mzuri wa kushirikiana katika utekelezaji kwa lengo la kuleta tija kwa nchi na wananchi wake”. Balozi Mwinyi alifafanua.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mashirika ya Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bw, Sylevester Mundanda alieleza kuwa Tanzania na Zambia zimejaliwa kuwa na maliasili lukuki kama vile ardhi, madini, maji na wanyama pori, hivyo, endapo kama zitatumiwa vizuri zinaweza kubadilisha uchumi wa nchi hizo kwa ajili ya kuwaletea maisha bora wananchi wake.
Alisisitiza umuhimu wa kukubaliana maeneo machache ya kipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji na ubunifu bila kusahau kujiwekea utaratibu wa kupima ufanisi kila baada ya muda.
Bw, Mundanda alihitimisha kwa kusema kuwa vikao vya JPC ni fursa nzuri kujadili changamoto za kiuchumi na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana nazo ili uchumi uweze kukua kwa faida ya wananchi wa pande zote.
|
Wednesday, February 24, 2016
Press Release
The President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr.
John Pombe Joseph Magufuli has sent congratulatory message to the President of
the Republic of Uganda, H.E Yoweri Kaguta Museveni following his re-election as the
President at the election held on February 18th 2016. The message reads as follows:
“H.E.
Yoweri Kaguta Museveni,
President-Elect
of the Republic of Uganda,
KAMPALA.
Your
Excellency and Dear Brother,
It
gives me great pleasure, on behalf of the Government and people of the United
Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, to extend to Your Excellency
our heartfelt congratulations on your re-election as the President of the
Republic of Uganda. Your re-election at the helm of your country is a true
reflection of the confidence that the people of Uganda have in you as well as a
testimony of their trust in your exemplary leadership.
I also take this opportunity to congratulate your party, National
Resistance Movement for its outstanding victory in the General Elections. As
you are well aware, both my party, Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the Government
of the United Republic of Tanzania have enjoyed brotherly relations with the
Ugandan people throughout the years.
While congratulating you on your well deserved re-election, I
wish to reaffirm my readiness and determination to continue working with you in
further strengthening our relations for the benefit of our two countries and
peoples.
Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the
assurances of my highest consideration”.
Issued by
the Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International
Cooperation
February 24, 2016
|
SERIKALI NA AKDN WAJADILIANA KUBORESHA MKATABA WA USHIRIKIANO
Maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (The Aga Khan Development Network- AKDN). Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine ambaye alifungua rasmi kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz P. Mlima. Kushoto kwa Balozi Sokoine ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka H. Luvanda ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa Serikali ya Tanzania. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kilipitia upya Mkataba wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na AKDN ambao ulisainiwa mwaka 2001. |
Kiongozi wa Ujumbe wa Mtandao wa Maendeleo wa Agakhan Dkt. Shakif Sachedina wa kwanza kushoto ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa AKDN akiwa na baadhi ya wajumbe wakifuatilia mazungumzo ya kikao. |
Sehemu nyingine ya wajumbe wa AKDN wakifuatilia kikao. |
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania walioshiriki kikao hicho ambapo Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa ilikuwa mwenyeji. Ujumbe wa Serikali ulihusisha Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Mamlaka ya Mapato Tanzania; Ofisi ya Rais Ikulu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wizara ya Sera na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. |
Balozi Joseph Sokoine akiagana na wajumbe wa AKDN baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi wa kikao hicho. |
Tanzania na Uturuki kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mhe. Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alipowasili nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa madhumuni ya kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki. |
Mhe. Dkt. Mahiga na Mhe.Cavusoglu wakiwa katika mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki |
Mazungumzo yakiendelea |
===========================================
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe.
Dr. Augustine Mahiga amefanya ziara ya kikazi nchini Uturuki tarehe 23 na 24
Februari, 2016.
Wakati
wa ziara hiyo Mhe. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Mhe. Mevlut Cavusoglu,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pembeni mwa Mkutano wa Mawaziri kuhusu
Somali, uliofanyika mjini Istanbul Uturuki tarehe 23na 24 Februari, 2016.
Katika
mazungumzo, Mawaziri hao walikubaliana kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina
ya Tanzania na Uturuki kwa kutilia mkazo mahusiano ya kibiashara na uwekezaji.
Aidha, Mhe. Waziri Mahiga aliwakaribisha Waturuki kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza
katika sekta ya kilimo hususan kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani mazao ya
kilimo.
Vilevile,
aliwakaribisha kuweka program za kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya kilimo
baina ya wataalam wa Uturuki na Tanzania.
Kwa upande
wake, Mhe. Cavusoglu alieleza kwamba Uturuki inaipa Tanzania kipaumbele kama
nchi ambayo ingependa kukuza mahusiano nayo ya kibiashara na uwekezaji. Pia alimkaribisha
Mhe. Waziri Mahiga na Tanzania kushiriki katika maonyesho ya biashara ya
Expo 2016 pamoja na maonyesho ya Soko la Afrika, hapo baadae mwaka huu.
Tuesday, February 23, 2016
Matangazo ya moja kwa moja kutokea Ngorongoro Crater yarushwa nchiniMarekani
Mwakilishi wa Serikali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara hiyo, Bw. Herman Keraryo akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea umuhimu wa matangazo ya moja kwa moja yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji la ABC News la nchini Marekani kutokea Bonde la Ngorongoro katika kuitangaza Tanzania. Shirika la ABC News kupitia kipindi chake mashuhuri cha Good Morning America kimerusha matangazo yake ya moja kwa moja kutokea Bonde la Ngorongoro tarehe 23 Februari, 2016.
|
Mhandisi Mkuu wa mawasiliano na matangazo wa Shirika la ABC News, Bi Farhoun akiwaeleza Wakurugenzi na Waandishi wa Habari namna matangazo hayo yatakavyorushwa kwa kutumia Teknolojia ya hali ya juu na kwamba wamejipanga kuwaonesha Wamarekani Wanyama na Jamii za Wamasai wanaoishi katika Bonde hilo. |
Bi. Farhoun akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Wakurugenzi |
Bi. Farhoun akielezea namna baadhi ya vifaa na mitambo inavyofanya kazi |
Wakurugenzi na Waandishi wa Habari wakiangalia namna matangazo yanavyorushwa moja kwa moja. Picha ya chini anayeonekana kwa mbali kwenye screen za televisheni ni mtangazaji mashuhuri wa kipindi cha Good Morning America, Bi. Amy Robach akizungumza wakati wa matangazo hayo |
Wakurugenzi wakisalimiana na sehemu nyingine ya Wataalam wa matangazo (crew) waliokuwa wamepiga kambi katikati ya Ngorongoro. |
Baadhi ya Wanyama walioonekana katika kipindi cha moja kwa moja cha "Good Morning America" |
Bi. Kasiga na Bw. Asante Melita kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Good Morning America Bi. Amy Robach. ===================================================
Shirika la Utangazaji la ABC News la nchini Marekani limefanikiwa kurusha matangazo yake ya moja kwa moja (live) kutokea Ngorongoro Crater kupitia kipindi chake maarufu cha “Good Morning America.”
Matangazo hayo ambayo yamerushwa tarehe 23 Februari, 2016 yanatarajiwa kutazamwa na watu milioni 5 Jijini New York na zaidi ya watu milioni 50 katika Marekani yote yanalenga kutangaza vivutio vya Utalii hapa nchini hususan Bonde la Ngorongoro pamoja na kuelezea jitihada za Serikali ya Tanzania katika uhifadhi wa mazingira na maliasili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kutokea Bonde la Ngorongoro mara baada ya matangazo hayo kurushwa, Mwakilishi wa Serikali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Herman Keraryo alisema kuwa kuna faida kubwa kwa matangazo hayo kurushwa nchini Marekani kwani ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuleta Watalii hapa nchini. Pia matangazo hayo ni moja ya jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto za kutangaza utalii ambapo njia hii iliyotumiwa na Shirika la ABC News ni nzuri kwani imefanikiwa kuwafikia watu wengi na kwa muda mfupi.
Bw. Keraryo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kutunza mazingira na Wanyamapori ambao wameendelea kuwa kivutio kikubwa cha utalii nchini.
“Kama mnavyojua utalii wa Tanzania bado unategemea wanyamapori kwa kiasi kikubwa pamoja na kuwa na vivutio vingine Kama vile mambo ya kale lakini bado wanyamapori wanatangaza zaidi utalii wetu hivyo ni wajibu wetu kuendelea kuwatunza” alisema Bw. Keraryo.
Mbali na Bw. Keraryo wajumbe wengine kutoka Serikalini walioshuhudia urushwaji wa matangazo hayo ni Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dkt. Freddy Manongi, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu, Dkt. Manongi alisema kuwa anaishukuru na kuipongeza Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Ubalozi wake wa New York, Marekani kwa jitihada za kulishawishi na kufanikisha shirika hilo la utangazaji kuja nchini na kwamba ana imani utalii utaongezeka kufuatia matangazo hayo. Alisema kuwa Tanzania imepata fursa nzuri ya kujitangaza bure kwa vile imekuwa ikutumia fedha nyingi kwa ajili ya kazi hiyo.
“Kitendo cha kuleta shirika la ABC News nchini kwa ajili ya kutangaza utalii ni cha kujivunia na pia ni fursa kubwa sana kwetu Watanzania. Hivyo napenda kuushukuru Ubalozi wetu New York kwani ninaamini kupitia matangazo haya tutafaidika sana na tunatarajia baada ya miezi michache kupata watalii wengi hususan hapa Ngorongoro” alieleza Dkt. Manongi.
Naye Bi. Kasiga, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alieleza jitihada zilizofanywa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania, New York pamoja na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika kufanikisha matangazo hayo ya moja kwa moja. Aliongeza kwamba jitihada hizo zitaendelea ikiwemo kuzitumia Balozi zetu zilizopo nje katika kuhakikisha vivutio vya utalii vya hapa nchini vinatangazwa duniani kote. Pia alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Mashirika mengine makubwa ya utangazaji duniani kuja nchini kutangaza vivutio hivyo.
Kwa upande wake Bi. Mdachi kutoka Bodi ya Utalii aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Tanzania ina Mabalozi wa hiari wa utalii watano nchini Marekani na kwamba matangazo hayo ya ABC News yatakuwa ni nyenzo mojawapo itakayotumiwa na mabalozi hao kuendelea kuitangaza Tanzania.
Naye Mwakilishi wa Shirika la ABC News Bi. Farhoun aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwawezesha kufanikisha matangazo hayo ambayo kwa namna moja au nyingine yataongeza watazamaji wa kituo chao kwa vile walihakikisha ni wanyama pekee wanaooneshwa kwenye matangazo hayo tangu mwanzo hadi mwisho.
Pia alisema kwamba wamevutiwa na hifadhi hiyo ya kipekee duniani na kuipongeza Tanzania kwa jitihada za utunzaji wa mazingira hususan Bonde la Ngorongoro na hawajutii uamuzi wao wa kuichagua Ngorongoro kwa matangazo hayo.
-MWISHO-
|
Subscribe to:
Posts (Atom)