Mhe. Dkt. Mahiga na Mhe.Cavusoglu wakiwa katika mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki |
Mazungumzo yakiendelea |
===========================================
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe.
Dr. Augustine Mahiga amefanya ziara ya kikazi nchini Uturuki tarehe 23 na 24
Februari, 2016.
Wakati
wa ziara hiyo Mhe. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Mhe. Mevlut Cavusoglu,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pembeni mwa Mkutano wa Mawaziri kuhusu
Somali, uliofanyika mjini Istanbul Uturuki tarehe 23na 24 Februari, 2016.
Katika
mazungumzo, Mawaziri hao walikubaliana kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina
ya Tanzania na Uturuki kwa kutilia mkazo mahusiano ya kibiashara na uwekezaji.
Aidha, Mhe. Waziri Mahiga aliwakaribisha Waturuki kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza
katika sekta ya kilimo hususan kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani mazao ya
kilimo.
Vilevile,
aliwakaribisha kuweka program za kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya kilimo
baina ya wataalam wa Uturuki na Tanzania.
Kwa upande
wake, Mhe. Cavusoglu alieleza kwamba Uturuki inaipa Tanzania kipaumbele kama
nchi ambayo ingependa kukuza mahusiano nayo ya kibiashara na uwekezaji. Pia alimkaribisha
Mhe. Waziri Mahiga na Tanzania kushiriki katika maonyesho ya biashara ya
Expo 2016 pamoja na maonyesho ya Soko la Afrika, hapo baadae mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.