Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) akizungumza na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya alipomwita Wizarani kufuatia taarifa za kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania na kundi la watu nchini India. Katika mazungumzo yao Balozi Mwinyi alisema Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo hicho. Pia alimtaka kufikisha ujumbe kwa Serikali yake ya kuchukua hatua kali kwa wote watakaopatikana na hatia ya tukio hilo na kuwahakikishia ulinzi Watanzania waliopo nchini India.Mazungumzo yalifanyika tarehe 04 Februari, 2016. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.