Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano na Vyombo vya Habari juu ya mafanikio yaliyopatikana katika Wizara ndani ya siku 100 za kwanza za Serikali ya Awamu ya Tano.
|
Dkt. Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Wizara katika kipindi cha siku 100 za kwanza za Serikali ya Awamu ya Tano. Mafanikio hayo ni pamoja na mchango wa Tanzania katika utatuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi; Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne za Afrika zilizochaguliwa wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na China (FOCAC) kwa China kuwekeza kwenye Viwanda; Kubana matumizi kwa kupunguza safari nje; na kuimarisha Balozi ili ziweze kuiwakilisha Tanzania kikanda na kimataifa. |
|
Waandishi
wa Habari wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Wizara na Mafanikio
yake ndani ya siku mia moja katika Serikali ya awamu ya tano. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.