Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiwa katika ya pamoja na Bi. Selma Kamm-Melai
(kulia) na Bw. Yohannes Ngomi- Kamm (wa pili kutoka kulia) Wawakilishi wa Kampuni
ya Utalii ya MAKASA SAFARIS iliyopo
Moshi, Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Utalii ya Holiday Fair 2016 (Vakatiebeurs 2016) yaliyofanyika hivi karibuni mjini
Utrecht. Kushoto ni Bi. Agnes Kiama Tengia,
Afisa Ubalozi.
Baadhi ya Makampuni binafsi ya Utalii
nchini Tanzania yalishiriki katika Maonesho hayo maarufu yanayofanyika kila mwaka
katika miji ya Amsterdam, Utrecht na Maastricht, Uholanzi ambapo huvutia maelfu
ya washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani. Maonesho ya Vakantiebeurs hutoa fursa kwa nchi kujitangaza hususan katika sekta
ya utalii. Ubalozi wa Tanzania ulihudhuria Maonesho hayo na kukutana na Wawakilishi
wa baadhi ya Makampuni hayo binafsi kutoka Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.