Wednesday, July 31, 2013

Thailand yatangaza mpango wa ushirikiano na Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa mkutano kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Thailand uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mhe. Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand ambaye alitoa msimamo wa nchi yake kuhusu Ushirikiano na Afrika.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa wakimsikiliza  Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo. Kulia ni Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar  na Bw. John Haule (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand, akitangaza rasmi mpango wa nchi yake unaolenga kuimarisha mahusiano kati ya Thailand na Afrika (The Thai-Afrika Initiative). Mpango huo utasaidia nchi za Afrika kushirikiana kwa karibu na nchi za Asia ambazo kwa siku za hivi karibuni zimekuwa na nguvu katika  uchumi wa dunia.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Sekta mbalimbali wakimsikiliza waziri Mkuu wa Thailand (hayupo pichani) akitangaza Mpango wa nchi yake wa kushirikana na Afrika.

Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi (katikati-msatari wa kwanza) kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto) na Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Waziri Mkuu wa Thailand (hayupo pichani).


Mhe. Shinawatra akitazama bidhaa za madini alipotembelea maonesho ya vito vya  madini mbalimbali yaliyoandaliwa na Wajasiriamali  Watanzania. Pembeni ni  Mhe.  Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji.


Mhe. Rais Kikwete nae akipata maelezo kutoka kwa Wataalam wa madini alipotembelea maonesho hayo.

Mhe. Rais Kikwete na  Mhe. Shinwatra wakijadili jambo kuhusu madini.

Mhe. Rais Kikwete akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu wa Thailand mara baada ya kutembelea maonesho ya madini na vito vya madini vinavyotengezwa hapa nchini. Kulia ni Naibu Waziri wa Nishari na Madini, Mhe. Stephen Masele (Mb.).


Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje akifurahia vazi la Khanga kutoka Thailand pamoja na wajumbe kutoka nchi hiyo.

Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni kutoka Thailand mara baada ya mkutano kumalizika.


Picha na Reginald Philip 

Tuesday, July 30, 2013

Tanzania na Thailand zasaini mikataba minne ya ushirikiano


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Ikulu na Waziri Mkuu wa Thailand, Mhe. Bibi Yingluck Shinawatra tayari kushuhudia uwekaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Waziri wa Fedha, Mhe. William Mgimwa (kulia) kwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Mhe. Dkt. Surapong Tovichakchaikul wakisaini Mkataba wa Kukuza na Kulinda Uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand.

Baadhi ya Wajumbe kutoka Thailand na Tanzania wakishuhudia uwekaji saini wa mikataba mbalimbali.

Mhe. Mgimwa na Mhe. Surapong wakibadilishana Mkataba mwingine kuhusu Ushirikiano wa Kitaalamu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Perreira Ame Silima (Mb.) (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Bibi Naomi Zegezege, Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria kabla ya kuanza kusaini Mkataba wa Kubadilishana Wafungwa kati ya Tanzania na Thailand. Pia Mhe. Dkt. Surapong akipokea maelekezo kama hayo kutoka kwa Afisa wa masuala ya Sheria kutoka Thailand.

Mhe. Silima na Mhe. Surapong wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini.

Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi kwa pamoja na Bibi Pornsawat Wathanakui, Mkurugenzi Mkuu kutoka Thailand wakisaini Mkatabakuhusu masuala ya Jiolojia na Usimamizi wa Rasilimali ya Madini.

Bw. Maswi na Bibi Wathanakui wakibadilishana mkataba mara baada ya kusaini huku Mhe. Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Thailand, Mhe. Shinawatra wakishuhudia.
 
Picha na Reginald Philip

Waziri Mkuu wa Thailand awasili nchini kwa ziara ya siku tatu

Waziri Mkuu wa Thailand, Mhe. Bibi Yingluck Shinawatra akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tatu hapa nchini.
Mhe. Shinawatra akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya ziara ya siku tatu.

Mhe. Shinawatra akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe, Said Mecky Sadick mara baada ya kuwasili nchini huku Mhe. Rais Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage wakishuhudia.

Mhe. Shinawatra akikagua Gwaride la Heshima.

Mhe. Shinawatra na mwenyeji wake Rais Kikwete wakisiliza nyimbo za mataifa yao zilipopigwa kwa heshima ya mgeni huyo.

Mhe. Shinawatra na Mwenyeji wake Rais Kikwete wakiangalia burudani ya ngoma iliyotolewa na moja ya kikundi kilichokuwa Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.

Mhe. Shinawatra  kwa pamoja na Mhe. Rais Kikwete wakisalimiana na raia wa Thailand waliopo hapa nchini waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu huyo alipowasili katika Hoteli ya Hyatt Regency.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule (kulia)  akiwa pamoja na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage (kushoto),  Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbwelwa Kairuki na Afisa Mambo ya Nje, Bw. John Pangipita wakibadilishana mawazo kuhusu ziara ya Waziri Mkuuu wa Thailand hapa nchini.


Picha na Reginald Philip

Monday, July 29, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UJIO WA WAZIRI MKUU WA THAILAND


220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Mkuu wa Thailand, Mheshimiwa Yingluck Shinawatra, anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho, tarehe 30 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya siku tatu nchini Tanzania  kwa mwaliko wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Bibi Shinawatra, ambaye atatokea Msumbiji, atalakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na mwenyeji wake, Rais Kikwete, na kupigiwa  mizinga 19 kwa heshima yake.

Wakati wa adhuhuri, Waziri Mkuu wa Thailand atafanya mazungumzo rasmi na Rais Kikwete, Ikulu na baadaye kutia saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Thailand.

Kabla ya kuhudhuria dhifa ya Taifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake, Ikulu, Bibi Shinawatra, ambaye anafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara takriban 70 wa Thailand, atahutubia mkutano wa Uwekezaji wa Biashara kati ya Thailand na Tanzania kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, ambao utahudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Thailand na wawekezaji wa ndani (Tanzania), Wanadiplomasia, Wasomi na Viongozi mbalimbali kutoka serikalini. Katika mkutano huo, Waziri Mkuu wa Thailand ataelezea sera ya uchumi ya nchi yake kwa Tanzania na Bara la Afrika. Baada ya hapo, Waziri Mkuu huyo atazuru maonyesho ya biashara hotelini hapo.

Katika siku ya pili ya Ziara yake, Mgeni huyo wa Taifa atatembelea Mbuga ya Wanyama ya Serengeti mkoani Mara, ambako atajifunza namna Mamlaka za Tanzania zinavyosimamia na kutunza Hifadhi za Taifa za Wanyamapori. Waziri Mkuu Shinawatra atakabidhi Vifaa mbalimbali vya kupambana na majangili kwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi za Wanyama (TANAPA).

Mgeni huyo atarejea Dar es Salaam tarehe 1 Agosti na kuagwa na mwenyeji wake, Rais Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uganda.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
Julai 29, 2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



 

Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati akutana na Wajumbe wa Umoja wa Vijana wa IYDU

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya akizungumza na Wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Kimataifa wa masuala ya Demokrasia (IYDU) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kuhusu nafasi ya Sera ya Mambo ya Nje katika kusimamia Demokrasia nchini. Vijana hao kutoka  nchi 19 za Mabara  yote Duniani wapo nchini kushiriki mkutano wa Bodi wa IYDU.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2013.

Baadhi ya Wajumbe wa IYDU  wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Balozi Yahya (hayupo pichani).

Bw. Aris Kalafatis ambaye ni Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Kimataifa wa Masuala ya Demokrasia (IYDU) akieleza madhumuni ya ziara yao hapa nchini.

Bw. Deogratias Munishi, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), akiwatambulisha kwa Balozi Yahya (hayupo pichani) Wajumbe aliofuatana nao kabla  ya mkutano kuanza.

Bw. John Heche Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), akielezea jambo wakati wa mkutano huo ambapo pia aliitoa shukrani kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuupokea Ujumbe huo wa Vijana.

Mmoja kati ya Wajumbe walio hudhuria, akiuliza swali wakati wa mkutano wao na Balozi Yahya.

Balozi Simba Yahya, akibadilishana mawazo na mmoja wa Wajumbe mara baada ya mazungumzo.

Balozi Simba Yahya akiwa katika Picha ya Pamoja, na Wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Kimataifa wa Maswala ya Demokrasia (IYDU) mara baada ya kumaliza mazungumzo nao. 

Sunday, July 28, 2013

Wizara yazungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally (mwenye suti) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Wizara katika kutekeleza  Diplomasia ya Uchumi. Wengine katika picha ni Balozi Simba Yahya (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia pamoja na Bibi. Zamaradi Kawawa, Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo na Mratibu wa Mkutano huo.
 
Bibi Kawawa akizungumza kabla ya kumkaribisha Bw. Mkumbwa kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza Bw. Mkumbwa (hayupo pichani) alipozungumza nao juu ya utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
Balozi Yahya (kushoto) akijibu moja ya swali lililoulizwa na Waandishi wa Habari.

Balozi Kairuki (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizotolewa naWaandishi wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.


Monday, July 22, 2013

Rais Kikwete aongoza Watanzania kuaga miili ya Askari 7 waliouawa nchini Sudan; Waziri Membe pia ahudhuria


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka saini kitabu cha maombolezi leo, mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisaini kitabu cha maombolezi mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezi.
 Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitafakari kwa kina tukio la mauaji wa Askari wa Tanzania lililotokea katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Wengine katika picha ni Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wa tatu kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Luteni Jenerali Samwel Ndomba (wa nne kushoto), Mnadhimu Mkuu wa Majeshi nchini.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (wa pili kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, naye alishiriki katika kuaga miili ya Askari 7 waliouawa nchini Sudan hivi karibuni. 

Mh. Waziri Membe akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Abdulrahman Kinana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Mhe. Rais Kikwete akizungumza kwa masikitiko wakati wa kuaga miili ya Askari saba wa kulinda amani waliouawa na waasi katika jimbo la Darfur, nchini Sudan hivi karibuni.  Rais Kikwete amevitaka vikosi vya ulinzi nchini kutokata tamaa kutokana na maafa hayo bali wazidishe moyo na kuendelea kulitumikia kwa ufasaha Taifa lao. 

Miili ya Askari wa kulinda amani wa Tanzania waliouawa katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ikiwasili kwenye Viwanja vya Diamond Jubilee tayari kwa kuagwa na wananchi, ndugu, jamaa na marafiki.

Simanzi na majonzi viliwatala kwa familia za Marehemu.

Mhe. Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa miili ya Marehemu.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) na Mke wa Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (katikati), pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakiwa kwenye majonzi mazito mara baada ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu hao.

Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Davis Mwamunyange akitoa saluti za heshima za mwisho kwa Marehemu hao.

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania,  Bw. Phillipe Poinso akitoa heshima za mwisho kwa Askari wa Tanzania wa kulinda amani waliouawa jimbo la Darfur nchini Sudan hivi karibuni.  Bw. Poinso alikuwa akimwakilisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.

Umati wa Wanajeshi na Wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Diamond Jubilee leo kuaga miili ya Askari hao saba.


Picha zote na maelezo kwa hisani ya Zainul Mzige wa www.dewjiblog.com