Wednesday, July 31, 2013

Thailand yatangaza mpango wa ushirikiano na Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa mkutano kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Thailand uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mhe. Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand ambaye alitoa msimamo wa nchi yake kuhusu Ushirikiano na Afrika.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa wakimsikiliza  Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo. Kulia ni Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar  na Bw. John Haule (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand, akitangaza rasmi mpango wa nchi yake unaolenga kuimarisha mahusiano kati ya Thailand na Afrika (The Thai-Afrika Initiative). Mpango huo utasaidia nchi za Afrika kushirikiana kwa karibu na nchi za Asia ambazo kwa siku za hivi karibuni zimekuwa na nguvu katika  uchumi wa dunia.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Sekta mbalimbali wakimsikiliza waziri Mkuu wa Thailand (hayupo pichani) akitangaza Mpango wa nchi yake wa kushirikana na Afrika.

Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi (katikati-msatari wa kwanza) kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto) na Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Waziri Mkuu wa Thailand (hayupo pichani).


Mhe. Shinawatra akitazama bidhaa za madini alipotembelea maonesho ya vito vya  madini mbalimbali yaliyoandaliwa na Wajasiriamali  Watanzania. Pembeni ni  Mhe.  Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji.


Mhe. Rais Kikwete nae akipata maelezo kutoka kwa Wataalam wa madini alipotembelea maonesho hayo.

Mhe. Rais Kikwete na  Mhe. Shinwatra wakijadili jambo kuhusu madini.

Mhe. Rais Kikwete akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu wa Thailand mara baada ya kutembelea maonesho ya madini na vito vya madini vinavyotengezwa hapa nchini. Kulia ni Naibu Waziri wa Nishari na Madini, Mhe. Stephen Masele (Mb.).


Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje akifurahia vazi la Khanga kutoka Thailand pamoja na wajumbe kutoka nchi hiyo.

Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni kutoka Thailand mara baada ya mkutano kumalizika.


Picha na Reginald Philip 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.