Konseli Mkuu Omar Mjenga wa Tanzania, Dubai pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani, Dubai wakionyesha makubaliano mara baada ya kumaliza kutiliana saini. |
Wednesday, November 26, 2014
Watanzania kupata punguzo la asilimia 40 kwa matibabu katika Hospitali ya Irani iliyoko Dubai
Tuesday, November 25, 2014
Rais Kikwete apokea salamu za kheri toka kwa Rais Obama
Rais Prof. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi Tanzania, nchini Marekani (Picha na Freddy Maro) |
Friday, November 21, 2014
Waziri Membe azindua Chama cha Urafiki wa Tanzania na China
Mhe. Membe akihutubia. |
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Yongqing akihutubia wakati wa hafla hiyo. |
Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Salim nae akizungumza wakati wa hafla hiyo |
Mhe. Membe kwa kushirikiana na Balozi Lu Yongqing wakizindua Chama hicho kwa mara nyingine. |
Waziri Membe, Balozi Lu na Dkt. Salim pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo. |
Waziri Membe pamoja na Wageni waalikwa wakiinua glasi juu kutakiana heri |
Waziri Membe akijadiliana jambo na Dkt. Salim |
Hafla ikiendelea |
WAZIRI MEMBE AWAASA WAHITIMU WA KIU KUTII SHERIA ZA NCHI
Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo.
PICHA NA Reuben Mchome
======================================
PICHA NA Reuben Mchome
======================================
Membe Mgeni Rasmi Mahafali KIU
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.
Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.
Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
Tuesday, November 18, 2014
PRESS RELEASE
Sultan of Oman, His Majesty Qaboos bin Said Al Said
PRESS RELEASE
His
Excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of
Tanzania has sent a congratulatory message to His Majesty Qaboos bin Said Al Said, Sultan
of the Sultanate of Oman on the occasion of the 44th Anniversary of
the Sultanate of Oman National Day.
The
message reads as follows;
“His
Majesty, Qaboos bin Said,
Sultan
of the Sultanate of Oman
MUSCAT,
Your
Majesty,
On
behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and
indeed on my own behalf, I would like to sincerely convey my warm
congratulations to you, Your Majesty and through you, to the Government and the
people of Oman on celebrating the 44th Anniversary of the National Day.
The
Sultanate of Oman and the United Republic of Tanzania have enjoyed cordial and
brotherly bilateral relations over the years. As you commemorate this joyous
occasion of your National Day, I wish to take this opportunity to reiterate my
Government’s desire and commitment to further enhance the traditional bond of
friendship and cooperation existing between our two countries for our mutual
benefits.
Please
accept, Your Majesty, my most sincere congratulations and best wishes for the
continued good health and happiness, and for the friendly people of the Sultanate
of Oman, further progress and prosperity”.
ISSUED BY: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL
COOPERATION, DAR ES SALAAM.
18th NOVEMBER, 2014
Monday, November 17, 2014
Waziri Membe afungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu Sayansi ya Jamii
Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo |
JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii. |
Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi huku wajumbe wakimsikiliza. |
Mhe. Membe (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano kuhusu masuala |
Waziri Membe akifurahia jambo na mmoja wa Wajumbe wanaoshiriki mkutano huo. |
Mhe. Membe akihojiwa na Wanahabari kuhusu mkutano huo. Picha na Reuben Mchome |
Saturday, November 15, 2014
Waziri wa Uchukuzi akutana na Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harrisson Mwakyembe (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo ofisini kwa Bw. Omar Mjenga, Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai.
Konseli Mkuu amemueleza Mhe. Mwakyembe kuhusu mazungumzo yake pamoja na Mhe. Gaith Alghaith, Mtendaji Ma wa Shirika la Ndege la FlyDubai, kuhusu mpango wa shirika hilo kuingia makubaliano ya ushirikiano pamoja na shirika la Ndege la Tanzania(Air Tanzania) ambako Flydubai watatoa ndege tano zitakazochukua njia za ndani (domestic routes) na zile za kikanda (regional routes).
Ushirikiano huu utasaidia kufufua njia zote za ATC na kuiwezesha ATC kuanza kupata mapato.
Njia za kikanda ni pamoja na Kinshasa, Lubumbashi, Goma, Kigali, Bunjumbura, Entebe, Nairobi, Sychelles, Moroni, Madagascar, Mauritius, Maputo, Lilongwe, Lusaka, Joharnessburg, na Harare.
|
Friday, November 14, 2014
Waziri Membe akutana na Mabalozi wa Misri na Sudan nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Misri hapa nchini, Mhe. Hossam Moharram alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. |
Mhe. Membe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Moharram. Wengine pichani ni Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri.......Waziri Membe na Balozi wa Sudan |
Waziri Membe akisalimiana na Balozi wa Sudan hapa nchini, Mhe. Dkt. Yassir Mohamed Ali alipokutana nae kwa mazungumzo Wizarani.
Picha na Reuben Mchome
|
Subscribe to:
Posts (Atom)