Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amefanya ziara ya Kikazi Nchi Rwanda na kuonana na Rais wanchi hiyo Mhe. Paul Kagame. Waziri Mahiga alifanya ziara hiyo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mahiga akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere mara baada ya kuwasili, amesema ziara hiyo ya kikazi nchini Rwanda ililenga kuonana na Rais wanchi hiyo Mhe. Paul Kagame kwakuwa ni jirani na ni mmoja wa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo pia walitumia fursa hiyo kujadili masuala mbambali kuhusu Jumuiya.
Aidha katika mazungumzo hayo walijadili suala la mgogoro wa kisiasa wa nchini Burundi na kwa pomoja kuangalia namna bora zaidi ya kurejesha amani ya kudumu katika nchi hiyo.
Pia Mhe. Waziri alipata fursa ya kuzungumza na wafanyabishara wa Nchini Rwanda ambapo wamesifu utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli. Wafanyabiashara hao wamesifu utendaji wa Serikali kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha utendaji wa taasisi zake ikiwamo Bandari. “Nimepewa salamu za pongezi na wafanyabiashara wa Rwanda nizilete kwa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri iliyofanywa na Serikali na wameahidi kuongeza ushirikiano wa kibishara baina ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Mahiga.
Vilevile Rais Mhe. Paul Kagame katika mazungumzo hayo amesisitiza ujenzi wa mradi wa reli ya ukanda wa kati ambayo itasaidia kukuza biashara zaidi baina ya nchi hizi mbili na kuongeza fursa za uwekezaji.
Mhe. Waziri akijadili jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga. |
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano. |
Wakizungumza mara baada ya kumaliza Mkutano na vyombo vya habari. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.