Wednesday, May 15, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa UNAMID

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Maalum na Msuluhishi  Mkuu wa  Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Darfur (UNAMID), Mhe. Mohamed Ibn Chambas mara baada ya kuwasili Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya namna Vikosi vya UNAMID vinavyotekeleza majukumu yake huko Darfur  katika kulinda Amani. Tanzania pia imechangia katika Vikosi vya UNAMID Wanajeshi wapatao  1,129.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Chambas.

Ujumbe uliofuatana na Mhe. Chambas akiwemo Meja Jenerali Wyjones Kisamba (wa tatu kushoto), Kaimu Kamanda wa Vikosi vya kulinda amani vya UNAMID kutoka Tanzania. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou.

Mhe. Chambas akimweleza Mhe. Membe jitihada mbalimbali zinazofanywa na UNAMID huko Darfur katika kuhakikisha amani katika Jimbo hilo lililopo Magharibi mwa Sudan inarejea.



Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Membe na Mhe. Chambas (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Nathaniel Kaaya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Togolani Mavura (kulia), Msaidizi wa Waziri na Bi. Eva Ng'itu (katikati), Afisa Mambo ya Nje.

Picha zaidi za mazungumzo hayo.

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Chambas baada ya kumaliza mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.