Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambao pia nchi zao ni Wanachama wa Kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Permanent 5) kuhusu hali inayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mhe. Membe pia aliwapa taarifa za kuitishwa kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) utakaofanyika mjini Kampala, Uganda tarehe 5 Septemba, 2013 kuhusu DRC. Nchi tano wanachama wa Baraza la Kudumu la Usalama la Umoja wa Mataifa ni China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Mkutano na Mabalozi hao umefanyika Wizarani tarehe 30 Agosti, 2013. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.