|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye Jukwaa la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. |
|
Mhe. Rais Kikwete akihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mjini New York ambapo katika hotuba hiyo alielezea masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafasi ya Tanzania katika kuchangia walinzi wa Amani, Mageuzi katika Umoja wa Mataifa, Utekelezaji wa Malengo ya Milenia na pia alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali ya Kenya kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea tarehe 23 Septeba, 2013 mjini Nairobi. |
|
Mhe. Membe akiwa na Mhe. Haroun Suleiman, Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar wkimsikiliza Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. |
|
Mhe. Ramadhan Mwinyi, Naibu Balozi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York akifuatilia hotuba ya Mhe. Rais kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy huku Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York akisikiliza kwa makini hotuba hiyo. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.