Monday, September 30, 2013

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, New York


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mjini New York alipofika Ofisini kwake kabla ya kukutana na Wafanyakazi wa Ubalozi huo.


Mhe. Membe akizungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Mjini New York (hawapo pichani) alipokuwa mjini humo kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mhe. Balozi Manongi akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao. Kulia kwa Balozi ni Bi. Rose Mkapa, Kaimu Mkuu wa Utawala Ubalozi akifuatiwa na Bw. Justine Kisoka na Bi. Ellen Maduhu, Maafisa katika Ubalozi huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy  wa kwanza kushoto akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, New York. Kushoto kwa Balozi Mushy ni Dkt. Justin Seruhere akifuatiwa na Bi. Maura Mwingira na Bw. Noel Kaganda Maafisa katika Ubalozi huo.

Bw. Yusuph Tugutu (kulia), Mhasibu wa Ubalozi akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)akifuatiwa na Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Mhe. Waziri, Bw. Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizarani na Bi. Tully Mwaipopo, Afisa katika Ubalozi.
 

Mazungumzo yakiendelea.
 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.