Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Iadara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York. |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News |
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO). |
Na Rosemary Malale, New York
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili
mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria
kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session
of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela
mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.
Kikao
hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia
kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General
Debate) ni “Post-2015 Development
Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa
kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.
Pamoja
na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe.
Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa
ikiwemo:- Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa
ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza
kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya
Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.
Mingine
ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya
Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake
na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza
kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa
Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban
Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa
Makampuni mbalimbali.
Aidha,
pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha
mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati
inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati
ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati
inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na
Kamati ya masuala ya Sheria.
Viongozi
wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe.
Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman;
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).
Wengine
ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu
Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa
Waandamizi kutoka Serikalini.
-Mwisho-
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.