Monday, September 23, 2013

Mhe. Rais aongoza kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye UNGA



 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongoza kikao cha kupokea taarifa za maandalizi kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb.) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.)
 
Mhe. Rais  Kikwete  akizungumza wakati wa kikao hicho huku Mhe. Membe akisikiliza. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Tuvako Manongi (kulia kwa Mhe. Rais), Mhe. Haroun Suleiman, Waziri wa Kazi, Zanzibar, Mhe. Terezya Huvisa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Annastazia Wambura (Mb. )na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatta Mulamula.
 
Mhe. Balozi Manongi akitoa taarifa fupi kwa Mhe. Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushierikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara  ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Robert Kahendaguza wakati wa kikao na Mhe. Rais Kikwete.
 
Maafisa wakati wa kikao hicho.
 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.