Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana alikutana na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje mjini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yake, Mhe. Waziri Membe alielezea yaliyojiri katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mjini Kampala, Uganda hivi karibuni.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe wakati wa mazungumzo nao jana.
Mhe. Waziri Membe akiendelea kuongea na waandishi, wakati Balozi Vincent Kibwana, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisikiliza kwa makini.
Mhe. Waziri Membe akiongea na waandishi wa habari.
Picha zote na Tagie Daisy Mwakawago
Waziri Membe aelezea kuhusu Mkutano wa ICGLR
Na Zainabu Abdallah
Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) wamemaliza kikao
chao kilichofanyika Jijini Kampala, Uganda 05/9/2013. Kikao hicho
kilijadili hali ya kuzorota kwa amani Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na M23 katika mji wa Goma.
Akioengea na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam 06
Septemba, 2013, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mheshimiwa Bernard Membe (Mb) alisema kuwa Wakuu wa Nchi walifikia
maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulaani vikali mashambulizi ya M23
katika mji wa Goma yaliyosababibisha vifo na majeruhi kwa raia na askari wa
kulinda amani.
Aidha, Wakuu wa Nchi na Serikali walitoa pole kwa Umoja wa
Mataifa na Tanzania kutokana na kifo cha Meja Khatibu Mshindo, mwanajeshi
wa Tanzania aliyeuwawa katika shambulio lililofanywa na Kikundi cha Waasi cha
M23. Katika shambulio hilo pia wanajeshi watano walijeruhiwa na hali zao
zinaendelea vizuri.
Vile vile, Mhe. Membe alisema kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa
ukiongozwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi za Maziwa
Makuu, Mhe. Marry Robinson upo Goma kuangalia hali ya usalama
Katika hatua nyingine, Wakuu wa Nchi waliagiza Serikali ya DRC na M23
kufanya mazungumzo ili kumaliza mgogoro huo kwa amani na kutoa siku 17
kukamilisha zoezi hilo. Siku tatu kati ya hizo ni kwa ajili ya
maandalizi na siku kumi na nne ni kwa ajili ya majadiliano na makubaliano ya
kufikia muafaka wa kumaliza mgogoro huo.
Kando ya mkutano huo, Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipata fursa ya kuongea
na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Katika mazungumzo hayo, Viongozi hao
waliazimia kudumisha na kukuza uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na
Rwanda.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.