Saturday, October 26, 2013

Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yafana

Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Miaka 68 ya Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo hufanyika tarehe 24 Oktoba ya kila mwaka. Mhe. Kagasheki alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwenye maadhimisho hayo.

Mhe. Kagasheki akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou mara baada ya kuwasili.

Mhe. Kagasheki akilakiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 68 ya Umoja wa Mataifa.

Mhe. Kagasheki akifuatana na Mkuu wa Itifaki, Balozi Maharage, Dkt. Kacou na Balozi Mushy kuelekea kwenye Jukwaa Kuu. (picha na Zainul Mzige wa dewjiblog.com)
Mhe. Kagasheki akisalimiana na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini mara baada ya kuwasili.
Mhe. Kagasheki akisikiliza Wimbo wa Taifa ukipigwa kuashiria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Gwaride la Heshima
Mhe. Kagasheki akikagua Gwaride la Heshima kwa ajili ya kuadhimisha miaka 68 ya Umoja wa Mataifa (picha hii na Bw. Zainul Mzige wa dewjiblog.com)
Mshereheshaji (MC) wa siku hiyo Bw. Macocha Tembele, Afisa Mambo ya Nje akiwa kazini
Viongozi wa Dini waliokuwepo uwanjani hapo.
Mabalozi na Wageni waalikwa mbalimbali pia walikuwepo.
Mabalozi
Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa DRC, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi wakifuatilia kwa makini maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Wageni waalikwa
Dua kuiombea amani dunia ikisomwa
Maombi yakitolewa
Sala ikitolewa 
Burudani kutoka Brass Band ya Jitegemee ikitolewa


Dkt. Kacou akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hiyo.


Wageni waalikwa wakimsiliza Dkt. Kacou (hayupo pichani)

Mhe. Kagasheki akihutubia

Dkt. Kacou na Balozi Mushy wakimsikiliza Mhe. Kagasheki (hayupo pichani)
Maafisa Mambo ya Nje wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani). Kushoto ni Bw. Lucas Mayenga, Bw. Amos Tengu na Bw. Tembele.

Maafisa wengine wakifuatilia maadhimisho hayo kwa furaha. Kutoka kulia ni Bi. Asha Mkuja, Bi. Ramla Khamis na Bi. Jubilata Shao.

Meza Kuu.

Mhe. Kagasheki akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho yaliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 68 ya Umoja wa Mataifa

Mhe. Kagasheki akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Taasisi zake.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Mkumbwa Ally akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Wizara kwa Mhe. Kagasheki alipotembelea Banda la Wizara.

Mmoja wa Maafisa kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Bw. Rodney Thadeus akitoa maelezo kwa Mhe. Kagasheki kuhusu utendaji wa kituo hicho.

Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo cha Diplomasia, Bw. Ali Masabo nae akimweleza Mgeni Rasmi, Mhe. Kagasheki majukumu ya chuo hicho

Bi. Praxida kutoka Taasisi ya APRM akimhudumia Balozi wa Msumbiji hapa nchini alipotembelea Banda la Wizara.

Mhe. Kagasheki akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkoma alipotemebelea mabanda mbalimbali Viwanjani hapo.

Dkt. Kacou akifurahia jambo na Balozi Mpango pamoja na Mkuu wa Itifaki, Balozi Maharage.

Balozi Mushy akisisitiza jambo kwa Dkt. Kacou.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.