Thursday, July 10, 2014

Mhe. Membe akutana na Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya FRELIMO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisalimiana  kwa furaha mgombea Urais kwa tiketi ya  Chama cha Ukombozi cha  FRELIMO cha  nchini Msumbiji, Bw. Filipe Nyusi ambaye ametembelea nchini kwa lengo la kutafuta kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania kufuatia kampeni za urais zinazoendelea nchini kwake . Waziri Membe alimwandalia chakula cha jioni katika Hoteli ya Hyatt Regency.
Mhe. Nyusi akisalimiana na Mbunge na Mfanyabiashara maarufu nchini, Mhe. Mohammed Dewji.
Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Marcel Escure
Waziri Membe akisalimiana na mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Samora Machel, Samora Samora ambaye aliambatana na mgombea huyo wa Urais.
Waziri Membe akimkaribisha Mhe. Filipe Nyusi na Ujumbe wake (hawapo pichani) katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa katika Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam
Mhe. Nyusi pamoja na wageni waalikwa wengine akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamim Nyanduga (kushoto) na Balozi wa Msumbiji nchini (wa tatu kushoto)  wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani)
Mhe. Filipe Nyusi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana  (kulia) na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga pamoja na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza Mhe. Filipe Nyusi (hayupo pichani)


Picha na Reginald Philip




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.