Thursday, July 10, 2014

Mhe. Membe akutana na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa iliyorithi shughuli za ICTR



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. John Hocking ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Bw. Hocking alitembelea Wizarani tarehe 10 Julai, 2014 kwa ajili ya kujadiliana na Mhe. Membe masuala mbalimbali ikiwemo mpango wa kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama hiyo katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
Maafisa waliofutana na Bw. Hocking wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Bw. Hocking nae akizungumza huku Mhe. Membe akimsikiliza.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju pamoja na Bw. Abdallah Mtibora wakimsikikliza Bw. Hocking (hayupo pichani).
Bw. Hocking akimuonesha Mhe. Membe Ramani ya Jengo la Makao Makuu ya Mahakama hiyo itakayojengwa katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
Mhe. Membe akimweleza jambo Bw. Hocking mara baada ya mazungumzo yao
Bw. Hocking akiagana na Balozi Kasyanju mara baada ya mazungumzo yake na Mhe. Membe.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.