Viongozi wapya wakiwa
katika picha ya pamoja na Balozi Kilumanga. Mwenye kanzu kushoto mwa Balozi, ni
Bw. Salum Ali Abdallah (Mwenyekiti), wakulia kutoka alipo Balozi ni Bw. Khalfan
Salum Khalifan (Makamu Mwenyekiti), anayefuatia kulia ni Bibi Rukia Selemani (Katibu).
Jana tarehe 10 Agost
2014, Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Visiwa vya Comoro walianzisha
rasmi Jumuiya yao. Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaunganisha
wanachama wake, kuwawezesha kushirikiana katika kutambua fursa za maendeleo na
kutoa mchango kwa taifa lao la Tanzania.
Mkutano huo ulifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi wa Tanzania, Moroni. Wakati akifungua
mkutano huo, Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro
aliwaeleza Watanzania hao kwamba Serikali ya Tanzania inathamini sana na
kutambua umuhimu wao Serikali imeanzisha Idara inayoshughulikia Watanzania
wanaoishi Ughaibuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Kitengo kama
hicho kimeanzishwa katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar. Sambamba na hilo, Viongozi
wote wamekuwa wakikutana na Watanzania wanaoishi Ughaibuni, kila wanapopata
fursa ya kufanya hivyo, wanapokuwa nje ya nchi. Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Nd.
Ali Jabir Mwadini alitoa mada kuhusu misingi ya uanzishaji wa Jumuiya za Kiraia
na kubainisha vipengele muhimu vinavyopaswa kuzingatiwa hususani katika katiba
ya Jumuiya.
Mwisho, ulifanyika
uchaguzi wa viongozi wa muda waliopewa jukumu la kuandaa katiba.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.