Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal,
akizungumza na Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe.Ali Said Siwa.
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo
amekutana na mabalozi wa Norway na Balozi mteule wa Tanzania nchini Rwanda na
kufanya nao mazungumzo ofisini kwake ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi wa
Norway nchini Tanzania mheshimiwa Hanne Marie Kaarstad ndiye aliyekuwa wakwanza
kufanya mazungumzo na mheshimiwa Makamu wa Rais ambapo licha ya kufika
kujitambulisha alimueleza mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa atajitahidi kuimarisha
uhusiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chake kama Balozi na kwamba
Tanzania ni nchi rafiki kwa Norway na akasisitiza kuzidi kuimarisha uhusiano
hasa katika masuala ya utunzaji wa mazingira.
Kwa upande
wake mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi Hanne kuwa, Tanzania
inajivunia uhusiano wake na Norway na kwamba uhusiano huo kwa sasa unazidi
kuimarika na tena Tanzania inategemea kujifunza mengi toka Norway kutokana na
nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye technolojia ya juu katika masuala ya
gesi na mafuta.
Balozi Hanne
ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania pia alionesha kufurahishwa kwake na
maendeleo ambayo Tanzania inapiga na kufafanua kuwa mji wa Dar es Salaam ni
kiashiria kimojawapo kinachoonesha wazi kuwa Tanzania inakuwa kwa kasi.
Pia,
Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpokea Balozi Ali Said Siwa aliyepangiwa kuwa
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda nakumtaka Balozi huyo kuhakikisha anasaidia
mahusiano baina ya nchi zetu kuzidi kuimarika huku akimsisitiza kuhusu uhusiano
wetu kama majirani na pia wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Balozi Siwa
alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa uteuzi wake na
akaahidi kuiwakilisha vema Tanzania nchini Rwanda.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.