Sunday, September 21, 2014

Waziri Membe aungana na Wana-Diaspora Marekani Kumuenzi Rais Kikwete kwenye "Usiku wa Jakaya"

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete kwenye meza kuu mara baada ya kuwasili kwenye "Usiku wa Jakaya" ambapo Watanzania waishio nchini Marekani - Diaspora walimpongeza kwa uongozi wake nchini Tanzania. Wengine kwenye meza kuu ni Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani na Bw. George Sebo, Mwenyekiti wa CCM Tawi la DMV, Marekani. 


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji wa "Usiku wa Jakaya" sherehe za kumpongeza Rais Kikwte kwa uongozi bora nchini Tanzania. Sherehe hizo zilifanyika kwenye Hoteli ya JW Marriott jijini Washington DC na kuhudhuriwa na vikundi mbalimbali vya Watanzania wanaoishi nchini Marekani.  
Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico wakifurahia jambo wakati wa sherehe za kumpongeza Rais Kikwete zilizofanyika tarehe 19 Septemba 2014, Washington DC nchini Marekani. 

Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo (ya kikombe) kutoka kwa Watanzania waishio Jimboni California wakiongozwa na Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa wakati wa kutoa zawadi. Mhe. Rais alipewa zawadi mbalimbali na vikundi vilivyowakilisha Watanzania kutoka Majimbo ya Minnesota, Illinois, California, North Carolina n.k.

Balozi Juma Maharage, Mkuu wa Idara ya Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Profesa Mohammed Janabi na wageni wengine waalikwa wakifuatilia sherehe hizo zilizofanyika kwenye Hoteli ya Marriott jijini Washington DC.

Balozi Joseph Sokoine, Mkuu wa Idara ya Ulaya na Marekani akiwa na Wasaidiza wa Rais na Wawakilishi wa Exxonmobil (wanaowekeza pia Tanzania) wakifuatilia sherehe hizo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatiafa  wakiwa kwenye sherehe za Usiku wa Jakaya

Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye picha na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Chakula na Dawa Tanzania Bw. Hiiti B. Sillo, baada ya sherehe za kumpongeza Rais Kikwete zilizoandaliwa na Watanzania wanaoishi nchini Marekani. 

Mhe. Bernard Membe akimpongeza Balozi wa Heshima Ahmed Issa baada ya sherehe za kumpongeza Rais Kikwete zilizoandaliwa na Wanadiaspora wa Tanzania nchini Marekani. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.