Mhe. Hamad akiwa na baadhi ya Masheikh na Viongozi aliofutana nao ================================================
Mhe. Seif Sharif Hamad, Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar amefanya ziara binafsi visiwani Comoro kuanzia
tarehe 1 hadi tarehe 4 Desemba 2014. Madhumuni ya ziara hii yalikuwa ni
kushiriki katika maadhimisho ya miaka arobaini (40) tangu kufariki kwa Marehemu
Sheikh Alhabib Omar bin Sumeti, mwanazuoni mashuhuri katika eneo la
Bahari
ya Hindi, ambaye aliwahi kuishi, kujifunza na kutoa elimu Visiwani Zanzibar.
Akiwa
nchini Comoro, Mhe. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipata pia fursa ya
kuonana na Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro,
na Mhe. Muhammad Ali Soilihi, Makamu wa Rais wa Comoro. Katika mazungumzo yake
na viongozi hao, Mhe. Makamu wa Rais alisifia juhudi zinazochukuliwa kuimarisha
uhusiano kati ya Tanzania na Comoro. Alibainisha kuwa zipo fursa nyingi za
ushirikiano ambazo endapo zitafanyiwa kazi, zitazinufaisha zaidi pande hizi mbili.
Aidha, Mhe. Seif Sharif Hamad alikutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi
Nchini Comoro na kuzungumza nao.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.