Monday, December 1, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Australia


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) ameagana na Balozi wa Australia nchini Tanzania Mhe Geoffrey Tooth ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. 
 Waziri Membe akizungumza na Balozi Tooth na kumweleza kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuiru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.
Mazungumzo yakiendelea kushoto wa kwanza ni Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo Bi. Freya Carlton.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa Australia ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.



Picha na Reginald Philip
==========================================

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo ameagana na Mhe.Geoffrey Tooth Balozi wa Australia nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. Katika mazungumzo yao. Waziri Membe alimueleza Balozi Tooth kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuiru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Balozi Tooth ambaye amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania kutokea Nairobi Kenya, kuanzia Desemba 2010 amemshukuru Mhe. Membe, uongozi wa Wizara na wafanyakazi wote kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote. Alisifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuleta maendeleo na kukuza mahusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine.

Balozi Tooth aliyeongozana na Bi. Freya Carlton, Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo, anatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kurejea Australia ambapo atakuwa mshauri wa Serikali kwenye masuala ya mazingira na mabadiliko wa tabia nchi. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.