MKUTANO NA BI. HENDERSON,
MKURUGENZI WA KITENGO CHA AFRIKA MASHARIKI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA
AUSTRALIA
Balozi
Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia amekutana na kufanya
mazungumzo na Bi. Henderson, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia leo tarehe 21 Mei 2015.
Katika
mazungumzo yao, waligusia juu ya maendeleo ya maandalizi ya ziara ya Dkt. Kim
Hames, Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Magharibi mwa Australia na Waziri wa Afya
na Utalii. Aidha Bi. Henderson aliipongeza Tanzania kwa kuandaa warsha na
mikutano ya kutangaza fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja
na uwekezaji katika sekta ya mafuta,
gesi na madini ambapo mwaka jana alihudhuria moja ya warsha iliyofanyika jijini
Adelaide, Australia.
Kwa upande wake Balozi Kairuki alichukua fursa
hiyo kuishukuru serikali ya Australia kwa nafasi za ufadhili wa masomo ya muda
mfupi na mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Afya.
Kwa
kuhitimisha, Balozi Kairuki alimweleza Bi. Henderson juu ya uwepo wa fursa
mbalimbali za uwekezaji nchini na kuwasihi wawekezaji kutoka Australia wasisite
kuja kuwekeza katika sekta ya madini, nishati na gesi nchini.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.