MKUTANO NA MKURUGENZI MKUU WA
IDARA YA HABARI NA DIPLOMASIA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA INDONESIA
Balozi
Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Habari na Diplomasia ya
Umma (Director General for Information and Public Diplomacy) kutoka Wizara ya
mambo ya Nje ya Jamhuri ya Indonesia, Balozi Esti Andayane.
Katika
mazungumzo yao, Mabalozi hao wamekubaliana kukuza ushirikiano baina ya
Indonesia na Tanzania katika nyanja za uchumi.
Balozi Andayane ameelezea utayari wa Indonesia kuendelea kuisaidia
Tanzania katika sekta ya Kilimo kwa kutoa fursa za mafunzo kwa ajili ya
wataalam wa kilimo nchini. Tayari
Indonesia imeisaidia Tanzania kwa kujenga Kituo cha Utafiti wa Kilimo kilichopo
Mkindo mkoani Morogoro. Aidha, katika mazungumzo hayo Balozi Andayane alitoa
taarifa kuwa serikali ya Indonesia imeisaidia Tanzania matrekta pamoja na vifaa
vyake. Tayari Wizara ya Kilimo imeshughulikia uingizaji wa matrekta hayo.
Kwa
upande wake, Balozi Mbelwa Kairuki aliishukuru serikali ya Indonesia kupitia
Mkurugenzi huyo kwa misaada mbalimbali wanayotoa kwa serikali ya Tanzania. Pia alishukuru
serikali ya Indonesia kwa kuialika Serikali ya Tanzania katika maadhimisho ya
miaka 60 ya ushirikiano kati ya bara la Afrika na Asia zilizofanyika Jakarta na
Bandung mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.