Wednesday, June 24, 2015

Katibu Mkuu Balozi Mulamula, Balozi Manongi na Balozi Gamaha wang'ara Nishani za Utumishi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula  
Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza. Hafla hiyo ilifanyika IKULU, Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza baada ya kumvisha Nishani
 ya Jamhuri ya Muungano Daraja la kwanza Balozi Liberata Mulamula
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Balozi Tuvako Nathaniel Manongi 
Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza. 
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mkono na Mhe. Tuvako Nathaniel Manongi 
 baada ya kumtunuku Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha Nishani
 ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Pili, Balozi wa Tanzania nchini Burundi Balozi Rajab Hassan Gamaha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza baada ya kumvisha Nishani
 ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Pili Balozi Rajabu Hassan Gamaha  
Wakuu wa Vyombo vya Usalama Nchini nao wakishuhudia utolewaji wa nishani za Jamhuri ya Muungano
Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchini zao nao wkiwemo katika ukumbi kwakushuhudia utolewaji wa Nishani hizo  
Kikundi cha Bendi ya Polisi kikitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa utolewaji wa nishani  
Kaimu Mkurugenzi Chuo cha Diplomasia Dkt. Bernard Archiula (kushoto) akifuatilia kwa makini utolewaji wa nishani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa mara baada ya kumaliza utoaji wa Nishani.
Watunukiwa  Nishani, Wakuu wa vyombo vya Usalama na wageni waalikwa wote wakiwa wamesimama kwa pamoja wakiimba wimbo wa Taifa
Balozi Mulamula akipongezwa na Dkt. Salim Ahmedi Salim kwa kutunukiwa Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la kwanza 
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimpongeza Balozi Mulamula kwa kupokea Nishani ya Jamhuri ya muungano Daraja la kwanza.
Rais Mstaafu Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Mulamula pamoja na ndugu waliokuja kumsindikiza wakati wa upokeaji wa Nishani  
Balozi Mulamula (Wa pili kulia), Balozi Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa vyombo vya usalama nchini.
Balozi Mulamula (Wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wake Balozi Simba Yahya (Wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (Wa kwanza kushoto mstari wa nyuma), Mkurugenzi Idara ya Ugavi Bw. Lucas Suka (Wa kwanza kulia mstari wa nyuma), Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Paul Kabale (Wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala, Bi. Glory Mboya (Wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Amisa Mwakawago (Wa pili kutoka kulia).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani za Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi (Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro (Wa tatu kulia)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu, Mhe. Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani za Jamhuri ya Muungano daraja la kwanza, Utumishi wa muda mrefu na maadili mema Daraja la Kwanza na Utumishi wa muda mrefu na maadili mema Daraja la Pili na Ushupavu Jumanne Juni 23, 2015 katika ukumbi mpya wa mikutano wa Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.