Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa Hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya kitaifa ya Taifa la Vatican pamoja na kuadhimisha miaka miwili ya Baba Mtakatifu, Papa Franci kuwa madaraki kwenye Ubalozi wa Vatican hapa nchini. Rais Kikwete ameipongeza Vatican kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania, pia alitumia nafasi hiyo kuwaaga Maaskofu wote wa Tanzania walio kuwepo kwenye maadhimishi hayo ikiwa ni sherehe yake ya mwisho akiwa madarakani. maadhimisho hayo yalifanyika katika makazi ya Balozi wa Vatican hapa nchini Askofu Padilla tarehe 26.06.2015, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe (Mb.), Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Bin Ally na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Mabalozi na maaskofu wa kanisa katoliki hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.