Balozi Yahya na Bibi Li wakibadilishana hati za makubaliano waliyosaini. |
Balozi Yahya na Bibi Li wakionyesha hati za makubaliano ya michoro ya Makao Makuu mapya ya wizara ya Nje. |
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeidhinisha michoro ya Makao Makuu mapya ya wizara hiyo, yatakayojengwa jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam.
Makubaliano kuhusu michoro hiyo ya jengo la ghorofa sita, litakalogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, yametiwa saini jana baina ya wizara na mwakilishi wa mkandarasi wa ujenzi.
Akiongea baada ya kutia saini makubaliano hayo kwa niaba ya wizara, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya, alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa matayarisho ya ujenzi kuanza, na kuwa kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa muhula wa Serikali ya Awamu ya Nne.
"Tumekamilisha hatua muhimu katika matayarisho ya ujenzi wa Makao Makuu mapya ya Wizara," alisema, na kuongeza kuwa mradi huu ulianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.
Utiaji saini wa makubaliano ya michoro hiyo ulishuhudiwa na wawakilishi wa Wakala wa Majengo (TBA).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.