Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Hailemariam Desalegn wakikata utepe kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya Mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda-TAMCO Kibaha Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 02 Julai, 2015. Wanaoshuhudia pembeni ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Tormo.
Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakizindua rasmi Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa Malaria. |
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kiwanda hicho.Wanaomsikiliza ni Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda na Mhe. Tormo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe.Hailemariam Desalegn akihutubia umati wa watu wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Kibaha.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi wa kiwanda hicho,wakimsikiliza kwa makini Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda, Mama Salma Kikwete na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichopo Wilayani Kibaha
Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza mstari wa mbele kulia) akiwa na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwa wamesimama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifurahia jambo na Mhe. Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho.
Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wataalam wa kiwanda hicho cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria
Juu na Chini ni baadhi ya mitambo ya kuzalisha Viuadudu hivyo vya kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria.
Picha na Reuben Mchome
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.