Friday, November 6, 2015

Balozi Mulamula awasindikiza Rais wa DRC na Msumbiji


Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama Kikundi cha Ngoma kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango 
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (mwenye pochi mkononi) akiagana na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi 
Rais Nyusi akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamimu Nyanduga.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye  anawakilisha pia nchini Algeria, Mhe. Begun Taj akimsindikiza Waziri wa  Nchi anayeshughulikia masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Algeria, Mhe. Ramtane Lamamra. Mhe. Lamamra alikuja nchini kwa ajili ya kuhudhiria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Lamamra akipanda kwenye ndege tayari kabisa kuanza safari ya kurejea nchini Algeria


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.