Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya Taifa la Oman yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Oman hapa nchini na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 24 Novemba, 2015. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Salim Ahmed Salim. Katika hotuba yake Balozi Yahya alisifu uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman na kuitakia heri nchi hiyo katika kuadhimisha miaka 45. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.