Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Vijana 12 wa Kitanzania kutoka Mpango utakaohusisha safari ya meli (the Ship for World Youth Program) kuzunguka nchi nne Barani Asia ambazo ni India, Sri Lanka, Singapore na Japan kwa lengo la kujadili masuala ya kijamii pamoja na mitazamo mbalimbali kuhusu mwingiliano wa tamaduni pamoja na kuangalia fursa miongoni mwa nchi mbalimbali. Mpango huo ulioandaliwa na Serikali ya Japan unatarajia kuanza tarehe 13 Januari hadi 02 Machi, 2016. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.