Friday, January 15, 2016

Waziri Mahiga mgeni rasmi Mahafali ya 18 ya Chuo cha Diplomasia

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), ambaye pia alikua mgeni rasmi wa Mahafali ya Kumi na Nane ya Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam, akifungua rasmi Mahafali hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 13 Januari, 2016.
Mgeni rasmi Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Balozi Mwanaidi Maajar wakiwaongoza wahitimu kuingia katika viwanja vya mahafali.

Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Mohamed Maundi akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali hayo.

Dkt. Watengere Kitojo, Mkurugenzi wa masomo chuoni hapo, akitoa neno la nasaha katika mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvand wakiwa na wageni wengine waalikwa waliohudhuria mahafali hayo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (aliyevua kofia), Bw. Lucas Mayenga wote kutoka Wizara ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa  wakiwa ni miongoni mwa wahitimu.
Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati), akiwatunuku wahitimu.
Baadhi ya wahitimu wakitunukiwa.

Baadhi ya wahitimu wakifurahia baada ya kutunukiwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (mbele kushoto), Msaidizi wa Waziri, Bw.Thobias Makoba (wa pili kutoka mbele), Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara, wakifuatilia Mahafali hayo.
Mhitimu Bw. James Bwana ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, akipongezwa na mgeni rasmi, baada ya kutangazwa kuwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo katika darasa lake.
Mke wa aliyekuwa Makamu wa Rais Awamu ya Nne, Bi. Asha Bilal (aliyevaa joho) naye alikua miongoni mwa wahitimu katika mahafali hayo.
Bendi ya Jeshi la Polisi, ikisherehesha Mahafali hayo.

Mgeni Rasmi wa Mahafali ya kumi na nane ya Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (MB), akikata keki, huku Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Balozi Mwanaidi Maajar(katikati), Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Mohamed Maundi (kushoto) huku Naibu Waziri, Dkt. Susan Kolimba (nyuma mwenye kitenge) wakifuatilia zoezi hilo.
zoezi la ukataji wa keki likiendelea.
Jukwaa kuu wakiongozwa na mgeni rasmi wakiwa wamesimama  kusikiliza wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Wahadhiri wa Chuo hicho nao wakiwa wamesimama  huku wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.


 Mgeni rasmi, Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na jukwaa kuu na wahitimu mara baada ya Mahafali hayo.
====================================
Picha na Reginald Philip.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.