Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Bw. KWON Hee-seog (hayupo pichani). Mazungumzo hayo rasmi ambayo yalijikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Korea Kusini yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2016. Wengine katika picha ni Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.