Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango, Maendeleo na Uratibu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, Bw. Theophilus Addey. Katika mazungumzo yao yalijikita katika kuelezea namna Serikali ya Tanzania inavyofanya kazi na Umoja wa Mataifa kupitia Mfumo wa One United Nations (One UN). Balozi Mushy alimweleza Bw. Addey kuwa Tanzania imekuwa nchi ya mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika utekelezaji wa mfumo huo tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2007. Bw. Addey ameambatana na ujumbe wa pamoja kutoa Serikali ya Liberia na Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.