Saturday, July 22, 2017

Wanaarusha wafurika katika amsha amsha ya kuchangamkia fursa za soko la EAC

Chuo cha Ufundi Arusha
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society-FCS), Bw. Francis Kiwanga alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi Arusha kwa ajili ya kufungua kongamano la siku moja la kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa za kibiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kongamano hilo ambalo lilikuwa na kaulimbiu "Chungulia fursa Boda to Boda" liliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, FCS na Clouds Media kwa udhamini wa Trademark East Africa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa ambapo pia alieleza sababu za kufanya kampeni ya kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za EAC. Bw, Kiwanga alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na FCS na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam zimebaini kuwa wastani wa vijana asilimia 11 katika nchi za EAC hawana ajira na asilimia 59 hawana taarifa kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo. Hivyo, Kongamano hilo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo ili vijana waweze kujiajiri.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akisoma hotuba ya ufunguzi ambapo alisisitiza umuhimu wa vijana kung'amua fursa mbalimbali na kubuni bidhaa zitakazokidhi soko la EAC lenye watu zaidi ya 150.

Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria kongamano hilo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Kaisi akitoa neno ambapo alihimiza vijana kujifunza elimu ya ufundi wa aina mbalimbali ili waweze kuwa wabunifu wazuri kutokana na teknolojia ya kisasa.

Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akitoa maelezo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za kufuata endapo mtu anataka kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashariki. Aidha, alisisitiza umuhimu wa vijana kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupata huduma kama za mikopo.

Watu wa makundi mbalimbali walishiriki kongamano hilo wakiwemo watu wenye mahitaji maalum. Pichani mlemavu wa masikio akipatiwa tafsri kwa lugha ya alama wa masuala yanayojiri katika shughuli hiyo.

Huwezi kufanya biashara katika nchi za EAC bila ya kuwa na Hati halali ya kusafiria. Pichani ni Bw. Suleiman Masoud, Afisa wa Uhamiaji akitoa maelezo namna ya kupata Hati ya Kusafiria. 

Mlemavu wa macho akitoa maoni yake na kuuliza swali kwa watoa mada. Alidai kuwa taasisi za Serikali ndio zinakwamisha na kuwachelewesha Watanzania wasiweze kuchangamki ipasavyo fursa za EAC kutokana na ukiritimba usiokuwa na sababu.

Kama kawaida ujumbe ulifikishwa kwa njia tofauti. Pichani ni wasanii wa bendi ya Cocodo wakicheza wimbo wa kuhamasisha biashara za kuvuka mipaka.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Vijana walifuatwa katika maeneo yao mtaani ili kufikishiwa neno la kuwahamasisha kufanya biashara za kuvuka mipaka ndani ya EAC. Pichani ni Mtaalmu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Abel Maganya akiwahamasisha vijana wanaofanya biashara zao kando ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Sehemu ya watu waliohudhuria wakisikiliza neno kutoka kwa Bw. Maganya.

Hamasa kwa njia ya muziki
Soko la Mbauda
Bw. Kisoka akitoa neno. Alisisitiza vijana waondoe khofu na wajiunge katika vikundi na aSerikali ipo nyuma yao kuwaunga mkono.

Wafanyabiashara wa Soko la Mbauda wakisikiliza ujumbe kwa makini.

Binti huyo akitoa ujumbe kwa njia ya ngojera ili mradi watu wahamasike na kuona umuhimu wa kujikwmua kimaisha kwa kufanya biashara za kuvuka mipaka.

Kinanda na gitaa vilipigwa kwa ustadi mkubwa na kutoa ujumbe kwa Watanzania wasibweteke kwni fursa zipo lukuki ktika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.