TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri
wa Nchi anayeshugulikia Masuala ya Afrika wa Uingereza kuzuru Tanzania tarehe
22 na 23 Agosti 2017
Waziri wa Nchi
anayeshughulikia Masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza,
Mhe. Stewart Rory atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini tarehe 22 na 23
Agosti 2017.
Mhe. Rory anakuja
nchini kwa madhumuni ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo la Uingereza (Department for International Development – DFID).
Aidha, wakati wa ziara
hiyo, Mhe. Waziri Rory amepangiwa miadi ya kuonana na Viongozi wa Serikali
akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga (Mb).
Baadhi ya miradi
ambayo, Mhe. Waziri ataitembelea ni upanuzi wa Bandari ya Dar Es Salaam, Shule
ya Msingi Mkoani, Bonde la Mto Msimbazi, Kiwanda cha Nguo cha Tooku kilichopo
katika Eneo la Viwanda la Benjamin Mkapa, Mabibo jijini Dar es Salaam na
kampuni ya Songas.
Waziri Rory pia
anatarajiwa kushiriki chakula cha mchana na vijana wa Kitanzania katika moja ya
migahawa `ya kawaida katika mitaa ya jiji la Dar Es Salaam
Baada ya kukamilisha
ziara yake, Waziri Rory ataondoka nchini tarehe 23 Agosti 2017 kurejea London.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Agosti 2017
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.