Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa BBC, Idhaa ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania, Bw. John Solombi leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. Timu ya BBC imeanza ziara kuwatembelea wadau wake wakubwa katika masuala ya kupashana habari na wameanza kwa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje na baadaye walielekea kwa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini. Katika mazungumzo hayo, wawili hao walikubaliana kufanya kazi kwa karibu kwa maslahi ya kuuelimisha na kuuhabarisha umma. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.