Friday, September 29, 2017

BBC Tanzania watembelea wadau wake


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa BBC, Idhaa ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania, Bw. John Solombi  leo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. Timu ya BBC imeanza ziara kuwatembelea wadau wake wakubwa katika masuala ya kupashana habari na wameanza kwa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje na baadaye walielekea kwa msemaji wa  Jeshi la Polisi nchini. Katika mazungumzo hayo, wawili hao walikubaliana kufanya kazi kwa karibu kwa maslahi ya kuuelimisha na kuuhabarisha umma.

Bw. Solombi akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
Mazungumzo yanaendelea. Katika picha anaonekana Bw. Aboubkar Famau, Mtangazaji wa BBC na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Vipindi, akichangia jambo katika mazungumzo hayo. Kulia kwake ni Bw. Ally Kondo, Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na aliyekaa peke yake ni Bi. Halima Nyanza, Mtangazaji wa BBC.

Picha ya pamoja

Timu ya BBC baada ya kukutana na  Kitengo cha Mawasiliano ilipata fursa ya kusalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb). Pichani anaoenekana Mhe. Naibu Waziri akiwapa neno la shukrani Team ya BBC kwa uamuzi wao wa kuichagua Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa mdau wa kwanza kutembelewa.

Mhe. Naibu Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Team ya BBC na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.