Thursday, January 18, 2018

Tanzania yawa mwenyeji wa Mkutano wa pili wa India - Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa pili wa India - Afrika uliofanyika katika ofisi za ubalozi wa India nchini Jijini Dar es Salaa tarehe 18 Januari 2017.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kumalizika tarehe 19 Januari 2018 ambapo umewakutanisha  wajumbe kutoka serikali ya India, wajumbe wa nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa lengo la kujadili masuala ya ushirikiano pamoja na kubuni maeneo mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa India na wa jumuiya hizo 

Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya akihutubia ambapo alieleza pamoja na kujadili masuala ya ushirikiano Serikali ya India itatumia fursa ya Mkutano huo kukusanya maoni, taarifa na mapendekezo yatakayotolewa na wadau hususan katika masuala ya ulinzi, amani na maendeleo ili kila Taifa liweze kufikia malengo ya kitaifa na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Waziri Mkuu Mstaafu, Dr. Salim Ahmed Salim akihutubia katika Mkutano huo ambapo alieleza kuwa India ni mfano wa Taifa kubwa linaloendeshwa kidemokrasia licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu na hivyo akasisitiza ni muhimu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika zikafata mfano huo ili ziweze kuruhusu shughuli za maendeleo kufanyika kwa amani na kuwaletea wananchi maendeleo.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza linaloshughulikia masuala ya Ulimwengu nchini India, Bw. Nalin Surie akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano huo ambapo alieleza India imejidhatiti katika kuhakikisha ushirikiano wake na mataifa ya Afrika unaimarika na kuwa wa manufaa kiuchumi huhusan kwa nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.
Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule (wa pili toka kulia) pamoja na wajumbe wengine wakifuatilia Mkutano.


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula wakifuatilia Mkutano. 

Sehemu ya wajumbe kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika wakifuatilia Mkutano.

Sehemu nyingine ya Wajumbe wakifuatilia Mkutano
Wajumbe wakishuhudia hafla ya ufunguzi wa Mkutano.

Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Mhe. Waziri Mahiga mara baada ya hafla ya ufunguzi kumalizika.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.