Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Prof. Pamalagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier ambapo pamoja na
mambo mengine, Balozi Clavier ameipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua
kupambana na janga a virusi vya corona nchini.
Balozi Clavier pia amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa
Ufaransa inaiunga mkono Tanzania kwa asilimia 100 kwa hatua ilizochukua
kupambana na janga la virusi vya corona na kusema Ufaransa itaipatia Tanzania
Euro milioni 30 ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu na riba ndogo kwa ajili ya
kupambana na janga la virusi vya Corona pamoja na kusaidia kuinua uchumi.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kabudi amemuelezea
Balozi wa Ufaransa jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika
kupambana na Janga la Corona nchini na kumhakikishia utayari wa Tanzania katika
kupambana na janga hilo na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania ilichukua hatua
hizo kulingana na hali halisi ya maisha ya watanzania.
Prof. Kabudi amesema hatua zilizochukuliwa na Tanzania
zililenga kuwafanya watanzania kuendelea na maisha yao bila ya kuathiriwa
kiuchumi huku wakijilinda na kuchukua tahadhari ambazo zilikuwa zikitolewa na
wataalamu wa afya nchini na duniani.
Balozi Clavier amemuambia Mhe. Waziri Kabudi kuwa Ufaransa
pia imetoa msaada wa Dola 500,000 ambazo watapewa wakulima wadogowadogo 6,000
nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo chao na maghala ya
kuhifadhia mazao yao.
Ameongeza kuwa Rais wa Ufaransa ameziandikia nchi za
G20 na Paris Club kuzishawishi kuahirisha ulipaji wa madeni na riba zake na pia
kufuta kabisa madeni hayo ili kuimarisha uchumi ambao umeathiriwa na janga la
corona katika nchi zinazoendelea.
Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi amekutana na
kuagana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutaglu ambaye amemaliza muda
wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake
kuwa atakuwa Balozi wa hiari wa Tanzania nchini uturuki na kwingineko duniani.
Naye balozi Davotaglu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini
na kuahidi kuwa ushirikiano uliopo utaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi ya kitabu cha
Mwl. Nyerere kutoka kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic
Clavier
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa
Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi
huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic
Clavier akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na
Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa Uturuki
nchini ambaye amemaliza muda wake wa utumishi, Mhe. Balozi Ali
Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja
na
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Balozi Ali
Davutaglu wakiangalia picha ya kazi zilizofanywa na Ubalozi wa Uturuki wakati
walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha Balozi
wa Uturuki nchini aliyemaliza muda wake wa utumishi, Mhe. Balozi Ali Davutaglu
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.