Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba kabudi (Mb) (wa kwanza kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Mawaziri pamoja na maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia
mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo
Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya mawaziri wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa
SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa
njia ya (Video Conference) leo
Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano huo
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi
wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano
na umoja wakati huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona huku bidhaa na huduma muhimu
zinazovuka mipaka baina ya nchi na zikiendelea kutolewa.
Prof. Kabudi amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano
wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya Video katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Nawaomba Nchi zote Wanachama wa SADC tuimarishe umoja na mshikamano wetu
wakati huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona, huku bidhaa na huduma muhimu
zinazovuka mipaka baina ya nchi nan chi zikiendelea kutolewa, huu ni wakati wa
kuepuka vitendo vya kujitenga na kuongeza mashauriano baina ya nchi,” amesema.
Aidh Mhe Waziri ameziomba
Nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva wanaosafirisha bidhaa
na huduma muhimu kuvuka mipaka ya nchi kwa wakati huu ambao ugonjwa wa corona
umeenea katika nchi wanachama.
Amesema Nchi wanachama zinapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na ueneaji
wa virusi vya Corona bila ya kuwanyanyapaa madereva na kuwachukulia kama watu
wanaosambaza virusi hivyo na kuongeza kuwa madereva hao wanapaswa kupewa
heshima stahiki kama binadamu wengine na kuwashukuru kutokana na hatari
wanayochukua ya kusafirisha mizigo na huduma wakati huu wa kuenea kwa janga
hilo.
“Madereva wetu wamevunjika moyo kwa sababu wanaonekana kama wao ndio wanaosambaza
virusi vya Corona na sio askari wazuri ambao wanatoa huduma ya kusafirisha
huduma na biidhaa muhimu wakati huu wa mlipuko, katika nchi za jumuiya,”
Ameziomba nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva hao
huku zikiendelea kuchukua tahadhari za kupambana na janga la virusi vya corona
na kuongeza kuwa umoja wetu ni muhimu sana kwa wakati huu.
“Naziomba nchi zetu tuwape heshima na kuthamini utu wa madereva hao na
kuwapa heshima wanayostahili huku tukiendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa
na wataalamu wa afya katika kukabiliana na janga hilo,” alisema.
Prof. Kabudi amesema janga la COVID 19 linaonekana kama halitoisha ndani
ya muda mfupi na nchi za ukanda wa SADC lazima ziishi kwa kufuata mifumo salama katika biashara na
usafirishaji wa huduma na bidhaa ili kupata ukuaji wa uchumi na kuondoa
umasikini huku tukiwa bado tunakabiliana na janga hili la ueneaji wa virusi vya
corona.
Amesema wakati hatua za
kukabiliana na janga la Corona zikiendelea kuchukuliwa nchi za SADC lazima
zikumbuke dhumuni la utangamano miongoni mwa nchi wanachama ambalo ni kuboresha
ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi na hivyo kutowaangusha waanzilishi wa
Jumuiya ya SADC.
Amesema ufanyaji wa
biashara baina ya nchi na nchi ndani ya SADC uko chini ya asilimia 20 hali
ambayo inazuia nchi wanachama kuona ukuaji wa uchumi wake na kuongeza kuwa
janga la corona lichukuliwe kama chachu ya kuongeza juhudi za kuinua
kiwango cha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi kupitia utekelezajia wa
Protokali ya SADC katika biashara ya 2005 na uanzishwaji wa eneo huru la
biashara la SADC.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwele na Waziri wa Maliasilia na
Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.